Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, October 12, 2014

Njia Moja Muhimu Ya Kuwa Kiongozi Bora.

Ni muhimu sana wewe kuwa kiongozi na ni muhimu zaidi kuwa kiongozi bora. Tunaposema ni muhimu wewe kuwa kiongozi haimaanishi kuwa kiongozi wa kisiasa au kiserikali bali ni uwe kiongozi kwenye jambo lolote unalofanya.

Iwe umeajiriwa kwenye kitengo fulani, fanya kazi yako kama kiongozi.

Iwe umejiajiri au unafanya biashara, fanya biashara yako kama kiongozi.

Iwe una familia, endesha familia yako kama kiongozi.

Ni viongozi pekee ndio wanaofikia mafanikio makubwa katika jambo lolote wanalofanya.

Hii ndio sababu kubwa imenifanya kuweka blog hii na kuandika kuhusu uongozi kila siku ya jumapili. Hii itatusaidia kujitengeneza na kuwa viongozi bora zaidi. Ili kuhakikisha hukosi makala hizi za uongozi weka email yako hapo juu na utakuwa unazipata makala hizi moja kwa moja kwenye email yako.

Ni ipi njia moja ya wewe kuwa kiongozi bora?

Njia moja ya wewe kuwa kiongozi bora ni kuwa mfuasi bora kwanza. Ni muhimu sana wewe kuwa mfuasi bora ndio wafuasi wako waweze kukuamini wewe kama kiongozi wao. Ni lazima kile unachotaka wafuasi wako wafanye, uanze kukifanya wewe kwanza.

Kumbuka watu hupenda vitendo zaidi ya maneno. Hivyo unavyoweza kufanya kwa vitendo ndio unavyoweza kuwahamasisha wafuasi wako nao kufanya kile unachofanya wewe.

Kuwa mfuasi bora kwa kufanya kile ambacho unataka wafuasi wako wakifanye na hii itakuongezea ushawishi mkubwa kama kiongozi.

Unataka kujenga maadili mazuri kwenye familia yako, hakikisha na wewe unakuwa na maadili mazuri. Unataka wafanyakazi wako wafanye kazi kwa bidii na maarifa, hakikisha na wewe unafanya kazi kwa bidii na maarifa.

Wewe kama kiongozi ni sehemu ya wafuasi wako, hivyo ni lazima uweze kuishi maisha ya wafuasi wako kama unataka kuwa na ushawishi mkubwa.

Nakutakia kila la kheri katika kujijenga kama kiongozi bora.

Usisahau kuweka email yako hapo juu ili kuhakikisha unapata makala hizi nzuri za uongozi.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment