1. Biashara yako haikui
Ili biashara yako ikue unahitaji kukua wewe kwanza. Kulalamika hakutakusaidia lolote. Anza kukua wewe na biashara yako itakua.
Utakua kwa kujifunza zaidi.
2. Una afya mbovu
Afya yako mbovu umeitengeneza wewe mwenyewe kwa tabia zako unazoendekeza. Inawezekana kula hovyo, kutokufanya mazoezi, kutokuzingatia kanuni za afya n.k
Badili yanayoharibu afya yako na itaimarika.
3. Umasikini wako
Kuzaliwa masikini sio kosa lako, maana huwezi kuchagua wazazi watakao kuzaa. Ila kufa masikini hilo ni kosa la kujitakia. Tumia uwezo, muda na mazingira yanayokuzunguka kuondokana na umasikini. Anza na kujifunza.
4. Hupendi kazi yako
Achana nayo na tafuta kitu unachopenda ukifanye. Ukilalamika tu haitakusaidia chochote.
5. Uko kwenye madeni
Moja ya sababu zilizofanya mpaka sasa uwe kwenye madeni ni kwamba una matumizi makubwa kuliko kipato chako. Hivyo hapa una mambo mawili ya kufanya; ongeza kipato chako au punguza matumizi yako. Ukiweza kufanya yote mawili utaona mabadilikonmakubwa sana.
Acha sasa kulalamika tu, Kama kuna chochote hupeni kibadilishe kama huwezi kukibadilisha achana nacho na usonge mbele.
Nakutakia kila la kheri, TUKO PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment