Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, November 9, 2014

Nguzo Kuu Ya Uongozi; Tekeleza Kile Unachoahidi.

Katika kujijenga kuwa kiongozi bora na imara kuna misingi mingi ya uongozi ambayo unatakiwa kuifuata. Kushindwa kufuata misingi hii kutapelekea uongozi wako kushindwa na hata kudharaulika sana.

Moja ya nguzo muhimu za uongozi ni kutekeleza kile unachoahidi. Kuongea ni rahisi sana na hivyo watu wengi hujikuta wakiongea mambo ambayo hawana uhakika kama wanaweza kuyatekeleza. Kwa kuwa kuongea ni rahisi watu hutumia nafasi hii kuongea mambo ambayo yatawafanya waonekane ni viongozi wazuri ila hawana uwezo wa kuyatekeleza.

Madhara ya kuahidi mambo usiyoweza kutekeleza.

1. Inakuondolea uaminifu.

Unapoahidi mambo halafu ukashindwa kuyatekeleza watu huondoa uaminifu kwako. Hivyo wakati mwingine utakapowaahidi hawatakusikiliza na hata wakikusikiliza hawataweka maanani uliyowaambia. Kwa sababu binadamu wana tabia moja kwamba ukishamdanganya mtu mara moja kila wakati atakuwa na wasi wasi na wewe.

2. Itakuondolea ushawishi.

Uongozi ni ushawishi, kama utaahidi mambo ambayo huwezi kuyatekeleza na kufanikiwakuwashawishi watu mara ya kwanza, baadae utapoteza ushawishi huo kama hukutekeleza yale uliyoahidi mara ya kwanza. Unapopoteza ushawishi unapoteza uongozi.

3. Unapoteza heshima yako.

Unapokuwa mtu wa kutekeleza maneno yako unaheshimika na wale unaowaongoza na hata jamii kwa ujumla. Unapoanza kuahidi mambo ambayo unashindwa kuyatekeleza unapoteza heshima yako.

Anza sasa kutekeleza kile unachoahidi kufanya, itakujengea sifa nzuri kama kiongozi na itakuongezea ushawishi na heshima mbele ya jamii.

Kama umeahidi wateja kwamba utawapatia bidhaa au huduma bora tekeleza ahadi yako.

Kama umewaahidi wafanyakazi wako kwamba wakifikia kiwango fulani cha uzalishaji utawaongeza mshahara basi timiza ahadi yako wanapofikia kiwango hiko.

Kama umewaahidi wananchi wakupigie kura ili uweze kuwasaidia kufikia maendeleo, tekeleza ahadi uliyotoa.

Hivi ndivyo unavyoweza kuwa kiongozi bora, TEKELEZA AHADI ZAKO NA IKIWEZEKANA ONGEZA ZAIDI.

Nakutakia kila la kheri katika uongozi wako.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment