Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, November 23, 2014

Mahitaji Manne Ya Mtu Kuwa Kiongozi.

Ili uweze kuwa kiongozi bora na mwenye mafanikio kuna vitu vinne unavyotakiwa kuwa navyo na uweze kuvisimamia. Kwa kujua na kusimamia vitu hivi kutakuwezesha kufanikiwa sana kama kiongozi.

1. Kuweza kujisimamia mwenyewe.

Kiongozi bora ni yule ambaye anayeweza kujisimamia mwenyewe. Ni lazima uweze kujiwekea malengo na mipango yako mwenyewe na uweze kuifuata bila ya kusimamiwa na mtu mwingine yeyote. Kama unahitaji kusimamiwa ndio uweze kutekeleza majukumu yako basi wewe sio kiongozi bali ni mfuasi. Na kama ukijaribu kuongoza kama unakosa tabia ya kujisimamia mwenyewe utashindwa vibaya sana.

2. Kuweza kutatua matatizo.

Kazi kubwa ya kiongozi ni moja, kutatua matatizo. Ili uweze kuwa kiongozi bora inabidi uweze kuyaangalia matatizo kwa jinsi gani yanaweza kutatuliwa. Kama unaogopeshwa na tatizo na kuona haliwezi kutatuliwa wewe sio kiongozi. Kila tatizo lina utatuzi wake. Ni kazi yako kama kiongozi kuja na njia za kutatua tatizo hilo na hivyo kuboresha hali iliyopo.

3. Kuweza kufanya mawasiliano mazuri.

Kiongozi bora ni yule ambaye anaweza kufikia ujumbe wake kwa watu anaowaongoza na wakauelewa na kuufanyia kazi ujumbe huo. Ili kuweza kufikisha ujumbe wao vizuri ni lazima uwe na mbinu nzuri za mawasiliano. Mawasiliano yanaweza kuwa ya maneno, maandishi au hata vitendo. Jinsi ambavyo unawasilisha ujumbe wako unaweza kuwa na ushawishi mkubwa au ukapuuzwa na wale wanaoupokea. Ni muhimu kujifunza mbinu bora za kufanya mawasiliano ili uweze kufikisha ujumbe wako na ufanyiwe kazi.

4. Kuweza kujenga mahusiano.

Kiongozi ni mtu na anayewaongoza ni watu. Ili uweze kuwa kiongozi bora ni lazima uwe na mahusiano mazuri na wale ambao unawaongoza. Kiongozi sio mtawala kwamba anachokisema yeye ndio mwisho, bali anahitaji kujenga urafiki na watu ambao anawaongoza. Kwa urafiki huu watu anaowaongoza watakuwa tayari kumshauri mambo mengi ambayo yatamsaidia kuongoza vizuri zaidi.

Hayo ndio mambo manne unayohitaji kuwa nayo ili kuwa kiongozi bora. Habari nzuri ni kwamba mambo yote hayo manne unaweza kujifunza na kuyaendeleza kwenye uongozi wako.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio yako kama kiongozi.

TUPO PAMOJA.

Tafadhali Washirikishe Wengine Makala Hii Nzuri!
SOCIALIZE IT →
FOLLOW US →
SHARE IT →
Powered By: BloggerYard.Com

0 comments:

Post a Comment