Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Tuesday, June 30, 2015

UKURASA WA 181; Kitu Cha Kufanya Pale Watu Wanapokuwa Hawakuamini Kama Unaweza.

Kama unataka kufanya jambo jipya, kama unataka kufanya jambo tofauti na wengine walivyozoea kufanya, naweza nikakuhakikishia jambo moja, WATU HAWATAKUAMINI.
Watu hawatakuamini kwamba unaweza kufanya jambo hilo. Watu hawatakuamini kwamba kuna uwezekano wa jambo hilo kufanyika kwa tofauti. Na hapa ndipo watu wengi hukata tamaa na kuamua kuacha. Na hivyo watu wale walioshindwa kuwaamini mwanzo wanakuwa sahihi na wanazidi kupata nguvu ya kuwaambia wengine kwamba hawawezi au haiwezekani.
Leo nataka nikuulize, je unajua unatakiwa kufanya nini pale ambapo watu hawakuamini kwamba unaweza? Au umekuwa mtu wa kukatishwa tamaa mara nyingi na wewe kukubali?
Sasa kuna kitu kimoja muhimu sana unachotakiwa kufanya pale ambapo watu hawakuamini kama unaweza. JIAMINI WEWE MWENYEWE. Wewe ndio umekuja na mawazo hayo uliyonayo, wewe ndiye ambaye umekuwa unafikiria usiku na mchana jinsi unavyoweza kubadili hali ya mambo. Wewe ndiye uliyefikiria na kuona kuna njia mbadala na ambayo inawezekana. Sasa kwa nini ukubali kumsikiliza mtu ambaye amefikiria kwa upande mmoja tu wa kwamba vitu haviwezekani?
SOMA; Hukuja Na Maelekezo Kwa Mtumiaji Na Kwa Nini Ufurahie Hili.
Kama utawasikiliza watu hawa utakuwa hujajitendea haki kabisa, kwa sababu hata watu hawa sio kwamba wana uhakika haiwezekani, ni vile tu hawajawahi kuona mtu mwingine akifanya hicho unachotarajia kufanya.
Kama watu hawaamini kwamba unaweza, huo ndio wakati wa kujiamini na hata kufurahia sana kwenye maisha yako. Unajua ni kwa nini? Kwa sababu unapoanza kufanya kitu ambacho wengi wanaona hakiwezekani, jua unafanya kitu ambacho sio cha kawaida, unafanya kitu kikubwa. Na mafanikio yanakuja kwa kufanya vitu ambavyo sio vya kawaida.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba pale ninapopanga kufanya jambo kubwa, watu wengi watashindwa kuniamini. Huu ni wakati muhimu sana wa mimi mwenyewe kujiamini na kuendelea kuweka juhudi. Hakuna mafanikio yanayokuja kwa kufanya vitu ambavyo ni vya kawaida. Hivyo ninapoona watu hawaniamini kwa kitu kikubwa ninachotaka kufanya, najua hapo ndio penye mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 182 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Monday, June 29, 2015

UKURASA WA 180; Pamoja Na Ushauri Mzuri Utakaopewa, Bado Kitu Hiki Utafanya Wewe Mwenyewe.

Unapokuwa unahitaji kufanya maamuzi ambayo huenda ni magumu kwenye kazi yako, biashara yako au hata maisha yako kwa ujumla, huwa unahitaji kupata ushauri. Unaweza kupewa ushauri mzuri sana kutoka kwa watu mbalimbali ambao unaweza kuwa unawaamini sana.
Pamoja na ushauri huu muhimu bado wewe mwenyewe ndio utahitaji kufanya maamuzi ya mwisho. Wewe ndio utakayekaa chini na kufanya maamuzi ambayo utakuwa tayari kuishi nayo.
Hivyo ni muhimu sana wewe uwe na uwezo wa kufanya maamuzi. Huwezi kutegemea tu watu watakavyokushauri, kwa sababu watu mbalimbali watakuwa na ushauri tofauti. Kama hutakuwa na uwezo mzuri wa kufanya maamuzi ambayo utakuwa tayari kuishi nayo, utaishia kufanya maamuzi ambayo yatakupoteza.
SOMA; Mambo Kumi(10) Unayotakiwa Kubadili Leo Ili Kufikia Mafanikio Makubwa.
Nakumbuka siku sio nyingi rafiki yangu mmoja aliniomba ushauri kuhusiana na maamuzi ya kibiashara aliyokuwa anataka kufanya. Nilimpa ushauri wangu na mambo muhimu anayohitaji kuzingatia. Baadae alinipigia kuniambia kwamba ameamua kufanya tofauti na nilivyomshauri. Nilistuka kidogo kwa sababu alichokuwa anakwenda kufanya ni kosa kubwa sana ambalo mimi binafsi nimewahi kufanya na likanigharimu na nimekuwa naona wengi wakifanya kosa hilo na linawagharimu sana. Nilijaribu kumwelewesha, labda kama hakuwa amenielewa vizuri, lakini alisisitiza kuendelea na kile alichopanga kufanya.
Nilijikumbusha kwamba yeye pekee ndio mwinye kufanya maamuzi ya mwisho na hivyo nilimwambia kila la kheri kama ndio maamuzi ambayo yuko tayari kuishi nayo. Siku chache baadae alinipigia na kuniambia hataendelea tena na mpango ule, hapa nilichanganyikiwa zaidi na sikutaka hata kujua zaidi.
Katika maisha yako jiandae kuweza kufanya mamauzi ambayo ni sahihi kwako na sio ya kusukumwa na mtu au kitu chochote.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba nitapata ushauri kutoka kwa watu wengi. Najua ushauri huu utakuwa mzuri sana, lakini mwisho wa siku ni mimi pekee nitakayehitaji kufanya maamuzi ambayo ni sahihi kwangu na nitakuwa tayari kuishi nayo. Kila siku nitajijenga ili niweze kufanya maamuzi ambayo yatakuwa bora kwangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 181 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Sunday, June 28, 2015

UKURASA WA 179; Unataka Kuwazidi Wengine? Umeshapotea.

Kwanza kabisa nikiri kwamba mimi huwa napinga sana dhana ya kushindana. Ndio kuna wakati ushindani unaonekana ni mzuri, lakini tatizo linakuja kwamba ukishakuwa na akili ya kushindana ndio unadumaa.
Kama unakuwa na akili ya kushindana maana yake lengo lako kubwa ni kuwazidi wengine. Kuwa wa kwanza, kuwa bora zaidi ya wengine.
Sasa tuseme labda unafanya biashara eneo ambalo watu wanafanya biashara kwa mitindo ya kizamani. Mtu akipata faida kidogo siku moja kesho yake analala, anaona amewini maisha. Na wewe ukawa unashindana nao, unafikiri utafika wapi?
Au tuseme unafanya kazi kwenye eneo ambalo kila mtu anakazana kununua gari na wewe ukawa na akili ya kushindana, unafikiri mafanikio yako makubwa kwenye maisha yatakuwa nini. Ukishanunua gari bora zaidi ya wengine tayari umekwisha. Utaonekana wewe ndio wewe na kile kiroho chako cha kushindana kitafurahi, kitakufanya uone maisha umeyamaliza.
SOMA; Sheria Tatu Muhimu Za Kufanikiwa Kwenye Maisha.
Lengo lako sio kuwa zaidi ya wengine, kama unataka kufikia mafanikio makubwa. Bali lengo lako ni wewe kuwa bora zaidi yako wewe mwenyewe. Wewe kuwa bora kuliko wewe mwenyewe. Wewe kuwa mbele yako mwenyewe. Hii ina maana kwamba leo uwe bora zaidi ya ulivyokuwa jana, leo ufanye kazi yako au biashara yako kwa ubora zaidi kuliko ulivyokuwa unafanya siku zilizopita. Leo upate kipato kikubwa zaidi ya ulichopata siku zilizopita. Leo upate mteja mpya tofauti na uliokuwa nao zamani.
Hiki ndio unatakiwa kupigania, hiki ndio unatakiwa kufanya kila siku. Na sio kuingia kwenye mbio za kundi na kujiingiza kwenye mashindano ambayo hujui hata yanakupeleka wapi.
TAMKO LA LEO;
Najua kukazana kuwa bora zaidi ya wengine ni kupoteza muda wangu na kujizuia kufikia mafanikio makubwa. Kuanzia sasa nitakazana kuwa bora zaidi yangu mwenyewe, nitakazana kuwa mbele yangu mwenyewe, kwa sababu najua kuna uwezo mkubwa uliopo ndani yangu ambao bado sijautumia. Nitahakikisha nautumia sasa ili niweze kufika mbali zaidi ya hapa nilipo sasa.
Tukutane kwenye ukurasa wa 180 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Saturday, June 27, 2015

UKURASA WA 178; Lakini Nitapitwa.... (Sababu Ya Kijinga Inayokufanya Upoteze Muda)

Kama umejitoa ili kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unahitaji kujifunza jinsi ya kutumia muda wako vizuri. Na kwa kuwa siku ina masaa 24 tu na hakuna anayeweza kuyazidisha, hakuna njia ya kuongeza muda ambao tunao.
Kwa kuwa tunahitaji muda mwingi zaidi wa kufanya kile tunachofanya kwa ubora, basi tunahitaji kupunguza mambo mengi tunayofanya ili tuokoe muda mwingi.
Ili kupata muda mwingi nimekuwa nawashauri watu kufanya yafuatayo, ambayo hata mimi nafanya; usifuatilie habari, punguza sana muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii, tenga muda wa kuwa mbali na simu yako pale ambapo unafanya kazi inayohitaji umakini wako.
Watu wamekuwa wakipinga sana baadhi ya mambo haya, hasa kutokufuatilia habari au kukaa mbali na simu. Watu wamekuwa wakisema lakini nitapitwa.....
Najua na wewe unaona usipoangalia au kusoma habari siku moja unaona unapitwa. Yaani unapitwa na habari ya mtu aliyejinyonga huko mpanda, ukishaisikia inakusaidia nini? Utaniambia kuna habari muhimu kuhusu mambo yanayoendelea. Kama habari ni muhimu kweli zitakufikia tu. Kwa mfano kama nchi inaingia vitani, utajua hata kama huangalii habari. Lakini mambo ya mgombea gani kapata wadhamini wangapi sio habari za mtu makini kushabikia, ni kupoteza muda wako.
SOMA; Unacho Kila Unachohitaji Ili Kufanikiwa.
Asilimia kubwa ya watu wanaotumia simu ni kama wamefunga ndoa na simu hizo. Kila dakika mtu upo na simu na hazipiti dakika tano unaangalia kama kuna mtu katuma ujumbe au kapiga hukusikia. Na hata unapokwenda kulala, unaiweka pembeni ya kichwa chako, ili usipitwe. Unapoteza muda mwingi sana, ni vigumu kufanya kazi yenye maana huku unajibu ujumbe wa simu au kupokea simu kila mara. Ni afadhali uweke simu hiyo kimya kabisa na ufanye kazi yako, bila ya kuiangalia. Utasema lakini watu watanipigia na kunikosa, nitakosa dili nzuri. Ukweli ni kwamba, na hapa nakuambia kwa uzoefu, kama mtu ana shida ya kuwasiliana na wewe kweli, atakutafuta hata mara kumi. Ila anayepiga mara moja na kuacha, hata ukija kumpigia baadae hakuna jambo kubwa na la haraka sana alilokuwa anakuambia. Mwingine atasema labda mtoto wangu ataumwa ghafla inabidi nipate taarifa, sawa umeshazipata unafanya nini? Maana hata kama wewe ni daktari huwezi kumtibu mtoto wako, itabidi apelekwe tu hospitali. Sisemi usikae na simu siku nzima, bali masaa machache hivyo taarifa hizi utazipata baadae na utafanya maamuzi sahihi, huku umeshakamilisha kazi uliyopanga kufanya.
TAMKO LA LEO;
Nimekuwa najidanganya kwamba nitapitwa na hivyo kuwa karibu na habari, kuwa karibu na mitandao na kuwa karibu na simu yangu kila mara. Hali hii imekuwa inanipotezea muda wangu mwingi kwa kufuatilia vitu visivyo na maana na kukosa muda w akufuatilia yale ambayo yataniletea mafanikio. Kuanzia sasa natenga muda wangu wa kufanya mambo muhimu na muda huu hautaingiliwa na kitu kingine chochote.
Tukutane kwenye ukurasa wa 179 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Friday, June 26, 2015

UKURASA WA 177; Ndio, Kwa Hiyo...

Ni vigumu sana kuweza kufanikiwa kwenye biashara, ndio kwa hiyo unahitaji kujipanga vizuri na kutokukata tamaa ili uweze kufikia mafanikio unayotarajia.
Umri wangu ni mdogo/mkubwa sana kuweza kuanza kufanya jambo hili sasa. Ndio kwa hiyo unahitaji kuwa wa tofauti, licha ya umri wako kuwa usiotegemewa bado unaweza kuweka juhudi na ukafikia kile ambacho unataka.
Nimejaribu mara nyingi sana lakini nimeshindwa. Ndio kwa hiyo unahitaji kubadili mbinu zako, kuendelea kufanya kitu kile kile na kutegemea majibu tofauti ni ujinga wa kupindukia.
Napenda sana kuanza biashara ila sina mtaji. Ndio kwa hiyo unahitaji kufikiria njia ya kuweza kuanza biashara kidogo au kutafuta kitu kingine cha kukuingizia kipato kwa sasa ili ujiandae na kuingia kwenye biashara unaotazamia.
SOMA; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya.... Na Madhara Yake.
Ukweli ni kwamba mtu yeyote anaweza kuja na sababu zaidi ya elfu moja kwa nini hawezi kufanya kitu fulani. Ila sababu hizi haziwezi kusaidia chochote.
Watu waliofanikiwa wanakuja na sababu lakini huzipatia sababu zao suluhisho ambalo hulifanyia kazi na hatimaye kufanikiwa.
Usiwe mtu wa kutafuta au kutoa sababu tu. Hebu anza kuzipa sababu zako suluhisho na utaona fursa nyingi sana za kukufikisha kwenye kile unachotaka.
Wakati wowote unapokuja na sababu tafadhali sana mbele yake ongeza NDIO KWA HIYO....
TAMKO LA LEO;
Najua sababu yoyote ninayojipa haiwezi kunifikisha kule ninakotaka kwenda. Ila ninapoifanyia kazi sababu ninayoipata ndio natoa nafasi kubwa kwangu kuweza kupata kile ninachotaka. Najua mjinga yeyote anaweza kuja na sababu kwa nini hafanikiwi na hii ndio inazidi kumfanya asifanikiwe. Lakini mimi sio mmoja wa wajinga hawa, kila sababu ninayopata lazima niipatie ufumbuzi.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Thursday, June 25, 2015

UKURASA WA 176; Hiki Ni Kipimo Kibovu Sana Cha Kupima Mafanikio Yako.

Kuna watu walikaa chini wakaamua kwamba kuwe na mtihani mmoja na wanafunzi wote waufanye, atakayepata maksi nyingi ndio amefaulu, atakayepata chache amefeli.
Kuna watu pia wamekaa wakakubaliana kwamba ukiwa na magari ya kifahari, ukawa na nyumba ya kifahari na fedha isipokuwa tatizo kwako basi wewe umefanikiwa.
Vyote hivi vinaweza kuwa vipimo kwa sababu vitakusukuma na wewe uweze kufika mbali zaidi ila sio vipimo sahihi kwa mafanikio yako. Hivi ni vipimo vibovu sana kwako kujipima kama umefikia mafanikio au la.
Hakuna kipimo kimoja kinachoweza kupima mafanikio ya watu wote kwa kigezo kimoja, ndio maana mara zote nimekuwa nakusisitizia sana usijilinganishe na wengine. Ni vizuri kujua wengine wanafanya nini, ila usijione umeshinda au umeshindwa kwa sababu ya kile unachofanya unavyokilinganisha na wengine wanavyofanya.
Kwa kifupi ni kwamba usipime mafanikio yako kwa vigezo ambavyo vimewekwa na watu wengine. Utakuwa hujitendei haki na kinaweza kuwa kikwazo kikubwa sana kwako kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Sasa ujipime na nini?
1. Jipimie kwa malengo makubwa uliyojiwekea? Je umeyafikia? Na kama hujayafikia ni kwa nini na umejifunza nini? Hakikisha malengo hayo ni makubwa; soma hapa kujua umuhimu wa malengo makubwa; Ni Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na Kushinda.
2. Jipime kwa juhudi unazoweka, je ni juhudi za kutosha? Je zinaleta matunda unayotarajia?
3. Jipime kwa ulivyokuwa jana na utakavyokuwa leo. je leo uko bora zaidi ya ulivyokuwa jana? Je kadiri siku zinavyokwenda unazidi kuwa bora au unazidi kuwa hovyo?
4. Jipime kwa maisha ya wengine uliyogusa. Je ni kwa kiasi gani watu wengine wamenufaika kwa kile ambacho unafanya? Je wataendelea kunufaika na kile unachofanya? Je watakukumbuka hata usipokuwepo?
Hivi ni baadhi ya vigezo sahihi kwako kujipima kama kweli umefikia mafanikio au la. Vigezo vinavyotengenezwa na wengine ni sumu kwako, usijaribu kuvitumia.
TAMKO LA LEO;
Nimekuwa napima mafanikio yangu kwa vigezo ambavyo vimewekwa na watu wengine. Njia hii imekuwa inaniumiza na kunirudisha nyuma. Kuanzia sasa nitapima mafanikio yangu kwa vigezo vyangu mwenyewe na nitahakikisha navifikia na kuweka vikubwa zaidi ili kila siku niwe bora zaidi ya siku iliyopita.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Wednesday, June 24, 2015

UKURASA WA 175; Ni Bora Kuweka Malengo Makubwa Na Kushindwa Kuliko Kuweka Malengo Madogo Na Kushinda.

Kwa jinsi tulivyolelewa na kukuzwa, kushindwa ni kitu cha aibu sana, ni kitu kinachostahili adhabu kubwa na kama utashindwa basi wewe ni mtu ambaye hufai. Si ndio tulivyofundishwa shuleni? Na ndio maana tulipewa adhabu kali pale ambapo tulishindwa kwenye kazi au mtihani.
Kinyume na ilivyo kwenye elimu na hata kwenye malezi uliyopewa, kwenye maisha ya kawaida kushindwa ni kitu kizuri sana. Kushindwa ni muhimu kwa sababu unajifunza mambo mengi kuliko unavyoshinda. Japo wengi hawaamini hili na hawataki hata kusikia.
Kwa woga wetu wa kushindwa, wengi wetu wamekuwa wakiogopa hata kuweka malengo makubwa kwa kuogopa kushindwa. Mtu anaona kama aliweka malengo makubwa na akashindwa kuyafikia basi ni sawa na kujidhalilisha. Kwa sababu hiyo anaweka malengo madogo ambayo yapo ndani ya uwezo wake na anayafikia vizuri.
SOMA; Hii ndio faida ya kushindwa.
Sasa kuweka malengo ambayo yako ndani ya uwezo wako na ukayafikia vizuri, unafikiri ni kitu gani kikubwa umejifuza? Hakuna, yaani umeendelea kuwa vile ulivyokuwa na huwezi kufikia mafanikio makubwa.
Lakini unapoweka malengo makubwa, malengo ambayo hata wewe mwenyewe yanakuogopesha, haya ndio malengo ambayo yatakusukuma ufanye zaidi na hata kama hutayafikia, utamaliza ukiwa mbali kuliko ungeweka malengo madogo.
Hivyo kuanzia leo na kwa muda wote uliobakia, malengo yote uliyoweka mwanzo yazidishe mara kumi na anza kuangalia ni njia gani zitakufikisha pale. Ndio weka mara kumi halafu umiza kichwa chako na weka juhudi mpaka tone la mwisho. Huenda hutafikia mara 10 lakini utafikia mara 5 au hata mara 3 ambayo ni bora zaidi ya kama ungeendelea na lengo lako la mwanzo.
TAMKO LA LEO;
Najua naogopa sana kushindwa, najua naona kushindwa ni kama aibu kwangu. Lakini nimeshajua kwamba kushindwa ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya kila siku. Kuanzia sasa nitaweka malengo makubwa na ambayo yatanisukuma kila siku ili kufanya zaidi ya ninavyofanya sasa. Kwa kuweka malengo makubwa hata kama sitayafikia nitajifunza na kuwa mbali zaidi kuliko nikiweka malengo madogo na ambayo naweza kuyafikia.
Tukutane kwenye ukurasa wa 176 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tuesday, June 23, 2015

UKURASA WA 174; Je Unafanya Kile Unachopenda Au Unachotegemewa Kufanya?(Na Mbinu Za Kuweza Kufanya Kile Unachopenda Kufanya)

Ni jambo la kushangaza kwenye maisha kwamba baadhi yetu tunaishi maisha ambao hata hatuyajui. Tunatumia muda wetu mwingi kuishi maisha ambayo hata hatukupanga kuyaishi. Tunajikuta tunaishi maisha tofauti kabisa kwa sababu tunalazimika kuishi maisha ambao kila mtu anaishi.
Tumeshazungumza sana kuhusu kuishi maisha ya wengine, leo ngoja tuzungumze kufanya kazi za wengine.
Kama imetokea kazi unayoifanya ikawa ndio kitu unachopenda kufanya upo kwenye nafasi nzuri sana. Na mafanikio yapo mbele yako. Ila ni nadra sana kuwa kwenye kundi hili ambalo lina watu wachache, asilimia 3 tu ya watu kwenye jamii.
Kama upo kwenye asilimia 97 iliyobaki, maana yake unafanya kazi unayofanya kwa sababu tu ndio unayotegemewa kufanya. Unafanya kwa sababu unafikiri ndio njia pekee ya kukupatia wewe kipato. Na kila mtu ameshakuaminisha hivyo na huwezi kuona nafasi ya kuondoka kwenye hilo.
SOMA; Mambo 20 Niliyojifunza Kwenye Kitabu Kinaitwa SELF-IMPROVEMENT 101.
Kama unafanya kile ambacho kila mtu anakutegemea ufanye, leo nataka nikupe mbinu ya kuanza kufanya kile ambacho unapenda kufanya.
Kwanza kabisa jua ni kitu gani unapenda, licha ya kazi ambayo sasa unaifanya. Amua ni kipi unapenda kukifanya na kila ukikifanya unajisikia vizuri sana. Iwe ni sanaa, iwe ni kitu cha kuwasaidia wengine, iwe ni mchezo na kadhalika. Chochote kile kinachokufanya ujisikie vizuri ni kitu muhimu sana kwako.
Baada ya kujua kitu hiki panga ni vipi unaanza kukifanya. Jua kwa sasa upo wapi na utaanzia wapi ili kufika wapi.
Kisha tenga muda kila siku wa kufanya kitu hiki. Kama kinahusiana na biashara, tenga muda kila siku wa kufanya biashara hiyo. Huna haja ya kuanzia mbali, anza kidogo na anza kwa kutafuta mteja mmoja, mpatie bidhaa au huduma nzuri na hakikisha unabadili maisha yake kupitia kile unachofanya. Tafuta tena mteja mwingine na fanya kama ulivyofanya kwa mteja wa kwanza na endelea kuboresha. Wakati huu bado unaendelea na kazi yako hivyo hujali sana kuhusu kipato, bali kutoa kitu bora ambacho kitawafanya wengine wakuzungumzie.
Ukiendelea hivi kwa muda, miaka kadhaa utafikia kuwa na wateja wengi kiasi kwamba kipato unachopata kwenye ajira yako ni kidogo ukilinganisha na hiki cha pembeni. Na hapo unakosa muda wa kuwahudumia wateja wako wote. Hapa ndio unaacha kazi na kufanyia kazi kitu hiko moja kwa moja.
Uko makini na umejitoa kutengeneza kitu kama hiki na unahitaji muongozo zaidi? Tuwasiliane, niandikie email kwenye makirita@kisimachamaarifa.co.tz na niambie ni nini unataka kufanya na tutajadili jinsi ya kuweza kupata muongozo mzuri. Ukiwa mwenyewe ni rahisi kukata tamaa, ukiwa na mwongozo utapata hamasa ya kwenda zaidi.
TAMKO LA LEO;
Najua ninachofanya sasa sio kile ambacho napenda kufanya bali ambacho kila mtu anategemea nifanye, ili nipate kipato cha kuendesha maisha. Sasa nimeamua kutenga muda kila siku na kuanza kufanyia kazi kile ambacho ninapenda kufanya. Nitaweka juhudi kubwa kwenye kitu hiki na najua kwa muda wa mbeleni kitakuwa chanzo changu kikubwa cha mapato.
Tukutane kwenye ukurasa wa 175 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Monday, June 22, 2015

UKURASA WA 173; Maamuzi Uliyofanya Awali Na Maamuzi Mapya.

Mambo unayofanya sasa yanatokana na maamuzi uliyofanya awali. Na maamuzi haya uliyofanya awali yalitokana na uelewa uliokuwa nao kwa kipindi hiko unafanya maamuzi hayo.
Sasa swali linakuja kwako je sasa hivi bado una uelewa kama uliokuwa nao kipindi unafanya maamuzi? Kama jibu ni ndio basi endelea na kile unachofanya.
Kama jibu ni hapana, maana yake uelewa wako ni tofauti na ulivyokuwa zamani wakati unafanya maamuzi. Je kwa kuwa na uelewa wa tofauti sasa upo tayari kubadilika na kufanya maamuzi mapya ambayo yatakuwa bora zaidi?
Hili ni swali la msingi sana nakuuliza kwa sababu watu wengi wakishafanya maamuzi na kuona mambo yanakwenda vizuri wanajisahau, wanaendelea kufanya kile walichozoea kufanya mpaka wanapojikuta kwenye wakati ambao wanachofanya hakifai tena.
Mtu anaingia kwenye kazi lakini anaendelea kufanya kazi yake kwa mbinui zile zile alizokuwa anatumia awali. Wanakuja vijana wenye mawazo mapya na wanaweka mbinu mpya na mtu huyu anaanza kuchukia na kuona nafasi yake ipo hatarini.
Mtu anaingia kwenye biashara lakini miaka nenda miaka rudi anafanya kwa mbinu zile zile, wakija watu wapya na mbinu mpya wanamwondoa kwenye biashara ile anabaki kulia kwamba kafanyiwa mchezo mchafu.
Kadiri uelewa wako unavyoongezeka, boresha maamuzi yako na fanya mabadiliko yanayostahili. Dunia inabadilika, ni lazima na wewe ubadilike. Nafikiri umeona hapo nimekuambia NI LAZIMA ubadilike, sio unaombwa, ndivyo dunia inavyokutaka, la sivyo unaachwa nyuma, unapotezwa.
Kama mpaka sasa hujasoma kitabu, JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA unasubiri nini? Bonyeza hayo maandishi kujipatia kitabu hiki kitakachokuandaa vizuri na mabadiliko.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba maamuzi niliyofanya awali yalitokana na uelewa wangu kwa kipindi kile. Najua kwamba mpaka sasa uelewa wangu umebadilika na hata dunia imebadilika pia. Nahitaji kufanya maamuzi mapya kulingana na mabadiliko ya sasa na uelewa nilio nao. Na kuanzia sasa mabadiliko kwangu yatakuwa ni mara kwa mara, sitafanya kitu chochote kwa mazoea.
Tukutane kwenye ukurasa wa 174 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Sunday, June 21, 2015

UKURASA WA 172; Tatizo La Kuweka Kinyongo...

Ni kwamba unakosa nafasi ya kufuatilia mambo mengine muhimu kwako.
Unaweza kujiaminisha kwamba kinyongo ulichomwekea mtu unastahili kabisa.
Alininyanyasa sana nilipokuwa mdogo...
Alinitesa sana katika mapenzi/ndoa....
Alinisababishia hasara kubwa kwenye biashara yangu...
Alisababisha kifo cha mtu muhimu sana kwangu....
Na sababu nyingine nyingi unazojipa kwamba kuweka kinyongo kwa mtu ni haki yako kabisa.
Lakini hebu niambie, kwa kuwa na kinyongo hiko kumekusaidia nini mpaka sasa? Je alichokufanyia mtu huyo kipindi hiko kimebadilika?
SOMA; SAMEHE…
Kukaa na kinyongo ni kuendelea kujitesa, kujinyima nafasi ya kufanya mambo ya msingi kwako na yatakayokupeleka kwenye mafanikio.
Na kinyongo hiko hakikusaidii wewe wala yule ambaye umemwekea.
TAMKO LA LEO;
Kuanzia leo nafuta vinyongo vyote ambavyo nimewawekea watu. Nimegundua vinyongo hivi haviniongezei chochote zaidi ya kunirudisha nyuma. Yeyote aliyenifanyia jambo baya sina muda wa kuendelea kumfikiria, nina maisha mengine mazuri ya kuishi na kufurahia. Sina nafasi ya vinyongo.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Saturday, June 20, 2015

UKURASA WA 171; Unapokata Tamaa Maana Yake Umekubali Hivi.

Kukata tamaa maana yake umeamua kuondoka kwenye safari inayokupeleka kwenye mafanikio.
Kukata tamaa maana yake umeamua kwamba nguvu zote ulizoweka, mambo yote uliyojitoa mpaka sasa hayana maana na umeamua kuyapoteza.
Kukata tamaa maana yake ni kusema ulikuwa hujui kile ulichopanga kufanya na hata sasa hujui ni kitu gani unataka kufanya kwenye maisha yako.
Kukata tamaa maana yake unaiambia dunia kwamba wewe huwezi kujitoa mpaka hatua ya mwisho.
Utakutana na mambo magumu sana.
Utakutana na changamoto nyingi sana.
Safari hii sio rahisi, ila pia kukata tamaa hakutakuletea urahisi wowote, zaidi kutakufanya ujisikie vibaya kwa kushindwa kufanikisha chochote.
Kamwe kamwe usikate tamaa, endelea kuweka juhudi, endelea kuboresha pale unapokosea. Hivi ndivyo utakavyoweza kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
TAMKO LA LEO;
Najua kukata tamaa ni kujidhalilisha kwenye maisha yangu. Najua kwamba safari hii sio rahisi, lakini pia kukata tamaa hakutarahisisha chochote. Nitaendelea kupambana mpaka nipate kile ninachotaka.
Tukutane kwenye ukurasa wa 172 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Friday, June 19, 2015

Kama unafuatilia blog hii kwa email, ukipata email hii nijibu.

Kama unafuatilia blog hii kwa email, ukipata email hii nijibu.
Habari za leo mpenzi msomaji na rafiki yangu?
Kwa siku za hivi karibuni nimepokea taarifa kutoka kwa baadhi ya wasomaji kwamba hawapati email za makala zinazowekwa kwenye blog hii Makirita Amani.
Mwanzoni nilifikiri ni tatizo la watu wachache ila kadiri siku zinakwenda nimekuwa napokea taarifa kutoka kwa wengi zaidi.
Nimejaribu kufuatilia mfumo unaotumika kutuma makala hizi moja kwa moja kwenye email ambao unamilikiwa na GOOGLE. Kuna baadhi ya changamoto nimeziona na hivyo nimezifanyia kazi.
Hivyo naomba kama utapata makala hii kwenye email yako ujibu ile makala ili nijue kama mambo yako vizuri.
Na baada ya hapo nitatuma link ya makala zote ambazo hazikutumwa ambazo ni kuanzia ukurasa wa 164.
Niombe radhi kwa usumbufu huu uliojitokeza na watu kukosa nafasi ya kufuatilia vizuri makala hasa za KURASA 365.
Makirita Amani.

UKURASA WA 170; Kinachoendelea Kukuzuia Kufikia Mafanikio Ni Hiki.

Kuna watu ambao wanakuwa wameanzia chini sana kwenye maisha. Wanatokea kwenye familia masikini, wanaweka juhudi nyingi sana na hatimaye wanafikia mafanikio waliyokuwa wanayatazamia. Ila baada ya kufikia mafanikio haya wanashindwa kwenda tena mbele na wanabaki palepale. Kwa kubaki palepale kwa muda mrefu wanajikuta wameachwa nyuma.
Kuwa wengine wanaingia kwenye kazi na wanaanzia ngazi ya chini kabisa. Wanakuwa na hamasa kubwa ya kwenda ngazi za juu na hivyo kuweka juhudi kubwa sana. Wanaweka juhudi hizi kweli na hatimaye wanafika ngazi za juu. Wanapofika pale wanafikia kikomo na hawaendi tena mbele.
Tatizo kubwa linalokufanya unashindwa kwenda mbele zaidi ya hapo ulipofika sasa ni kuendelea kufanya kile ambacho kimekufikisha hapo ulipo. Sikiliza, kile kilichokufikisha hapo ulipo, ndio kitakufanya uendelee kuwa hapo ulipo. Kama unataka kwenda mbali zaidi ya hapo ulipo sasa, unahitaji kufanya kitu cha tofauti na unachofanya sasa.
SOMA; Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja.
Watu wengi wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea. Utawasikia, hivi ndivyo nilivyofanya na nikafanikiwa, lakini ukweli ni kwamba mafanikio wanayoongelea ni ya miaka mitano iliyopita. Kama mafanikio unayoongelea sio ya wiki iliyopita au mwezi uliopita, tafadhali sana kaa kimya. Labda nirudie tena kwa msisitizo, kama unajisifia kwa mafanikio uliyopata miaka miwili iliyopita basi umeshapotea. Kama unajisifia kwa mafanikio haya ya mbali basi hakikisha una mengine ya juzi juzi ya kusemea pia.
Adui wa wewe kwenda mbele zaidi ni hapo ulipo sasa, na anaanza kwa kufanya vitu kwa mazoea kwa sababu ulishaozea kufanya hivyo. Mambo yanabadilika kila mara, kilichokufikisha hapo hakitakupeleka mbele zaidi. Unatakiwa kujua vipya na kuvifanyia kazi.
Kama bado hujasoma kitabu JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, kisome sasa. Kukipata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu 5 na email yako kwenye namba 0717396253/0755953887 kisha utatumiwa kitabu hiki kizuri sana. Usikose nafasi hii nzuri ya kunufaika na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwenye maisha yako ya kila siku na kuweza kufikia mafanikio makubwa.
TAMKO LA LEO;
Najua ya kwamba kilichonifikisha hapa nilipo, hakitaweza kunifikisha mbali zaidi. Najua kutumia kile nilichozoea kufanya kufika mbele zaidi ni kupoteza muda. Nahitaji kubadilika, nahitaji kuja na njia mpya kila siku ili niweze kunufaika na mabadiliko yanayotokea kwenye maisha.
Tukutane kwenye ukurasa wa 171 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Thursday, June 18, 2015

UKURASA WA 169; Utaendelea Kuidhulumu Dunia Mpaka Lini?

Kila mmoja wetu ana kitu kikubwa sana ambacho kipo ndani yake, ambacho akikitoa anaweza kuleta mabadiliko makubwa sana kwa watu wengine. Lakini tatizo kubwa ni kwamba wengi wetu hatutoi vitu hivi. Na tumekuwa tunaidhulumu dunia kwa kiasi kikubwa sana.
Kazi ambayo nimekuwa naifanya, ya uandishi na kufundisha, imekuwa inawasaidia watu wengi sana. Najua hili kwa sababu wengi wamekuwa wakiniandikia jinsi ambavyo maisha yao yanabadilika. Wakati naanza kuandika, nikiwa bado nakazana kutafuta njia gani ya uandishi ninaipendelea na nitapata watu wa kunisikiliza na kufanyia kazi kile ninachoandika, kuna wakati niliona hakuna kikubwa kwenye uandishi huu, nafanya kwa sababu napenda tu kuandika. Ila kwa sasa, kama nikisema niache kuandika leo, nitakuwa nimefanya dhuluma kubwa sana kwa dunia hii. Ni jukumu langu kuendelea kutoa maarifa ambayo yanawawezesha watu kubadili maisha yao, na kuyafanya yawe bora zaidi ya yalivyokuwa hapo awali.
Hata wewe pia una kitu kikubwa cha kutoa kwenye dunia hii. Kupitia biashara au kazi unayofanya, usiangalie tu ni mshahara kiasi gani unapata, usiangalie tu ni faida kiasi gani unapata, angalia ni thamani gani unatoa kwa wengine. Angalia ni jinsi gani unayagusa maisha ya wengine. Fanya hivi kwa moyo mmoja na kwa juhudi kubwa na ninakuhakikishia, ndio nakuhakikishia kwamba dunia italazimika kukulipa, na itakulipa kwa kiwango kikubwa sana mpaka mwenyewe utashangaa muda wote ulikuwa wapi hukulijua hili.
SOMA; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya.... Na Madhara Yake.
Wewe ni mwandishi? Andika mpaka mtu ashawishike kufanya kile unachoamini ni sahihi kwake kufanya, na atakapofanya na akafanikiwa, atakulipa, kwa kiwango kikubwa sana.
Wewe ni muimbaji? Imba mpaka watu wasimame, watu waache kufanya wanachofanya wakusikilize, watu watafute wimbo wako wakati wanajisikia kukata tamaa, na wautafute pia wakati ambapo wana furaha na watakulipa sana.
Wewe ni mwalimu? Fundisha mpaka watu waelewe, hakikisha hakuna anayetoka akiwa mtupu na hata kama haelewi lile somo unalomfundisha basi hakikisha unamfundisha chochote kitakachomsaidia kwenye maisha.
Wewe ni daktari? Toa huduma nzuri za afya zitakazookoa na kuboresha maisha ya watu. Fanya kila unachoweza kuhakikisha kwamba mgonjwa anayekuja kwako akiwa amekata tamaa kwamba maisha yake ndio yanafika tamati, aondoke akiwa na maisha yenye matumaini, hata kama huwezi kumponesha, basi umpunguzie hata maumivu. Na dunia italazimika kukulipa.
Hakuna kitu kizuri ambacho utakifanya na dunia ikaacha kukulipa, nina uhakika na hili. Nakusihi sana, fanya leo. Hata kama ni mzazi, toa malezi bora kwa mtoto wako na wanaokuzunguka pia, dunia itakulipa.
TAMKO LA LEO;
Najua nimekuwa naidhulumu dunia kwa kushindwa kutumia uwezo mkubwa ambao upo ndani yangu. Kuanzia sasa nitafanya kile ninachofanya kwa moyo mmoja na kwa ajili ya kufanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi. Najua dunia itanilipa kwa hili na fedha haitakuwa tatizo kubwa kwangu. Kila siku nitaikopesha dunia kwa kufanya mambo ambayo ni bora na najua dunia italazimika kunilipa.
Tukutane kwenye ukurasa wa kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Wednesday, June 17, 2015

UKURASA WA 168; Kama Umeshaanza Kutumia Kauli Hizi Sahau Kuhusu Mafanikio.

Enzi zangu mimi bwana, hela ndogo ndogo kama hizi zilikuwa hazinipigi chenga.....
Enzi hizo nilikuwa msanii maarufu sana sema basi tu sasa hivi mambo yangu hayako vizuri...
Enzi zangu biashara niliyokuwa nafanya ilikuwa na mafanikio makubwa sana. Sema sasa hivi tu mambo hayajakaa vizuri.....
Enzi hizo kazini mimi ndio nilikuwa kila kitu, ila hawa vijana wa siku hizi wamekosa heshima na kunichukulia mtu wa kawaida tu.....
Kama umeshaanza kutumia moja kati ya kauli hizo hapo juu nikupe pole kwa sababu umeshaondoka kabisa kwenye njia itakayokupelekea kwenye mafanikio. Ila nikupe moyo kwamba kama utasoma hapa na kama umekuwa unasoma makala nyingine kupitia mtandao huu basi una nafasi ya kubadili maisha yako.
Kauli hizo hapo juu ni dalili ya kukata tamaa, dalili ya kushindwa na dalili kwamba hakuna kitu kikubwa kinachoweza kutokea mbele yako. Kauli hizi zinatokana na mtu kufikia mafanikio fulani na kujisahau, kwa kujiona yeye ndio yeye n hivyo anaacha kujifunza na kuendelea kuweka juhudi. Baada ya muda mtu huyu anaachwa nyuma na kujiona kwamba hawezi tena.
SOMA; Kauli Mbili Za Kuacha Kutumia Leo, Maana Zinaashiria Kushindwa.
Kama wewe ni mmoja wa watu hawa, napenda kukuambia kwamba anza leo kufanya tena kile ambacho ulikuwa unafanya. Acha mara moja kutumia kauli za enzi hizo na fanyia kazi kile ambacho unataka kuwa vizuri. Haijalishi una miaka 20 au 50 au 80 kama unajua kitu ambacho ulikuwa bora ila kwa sababu fulani ukajisahau, anza kukifanya tena. Anza kujifunza kuhusu kitu hiki, anza kuweka tena juhudi, weka ubunifu na usikate tamaa.
Kwa kufanya hivi utaanza kuona mabadiliko, utaanza kuona watu wakiheshimu tena vile viwango vyako na utarudi kwenye ngazi zako za mafanikio.
Acha kutumia kauli zinazoonesha kwamba jana yako ilikuwa bora kuliko leo, pambana kila siku inayokuja uwe bora zaidi kwenye kile unachofanya. Kama ilivyo kwa miti kwamba inaendelea kukua mpaka pale inapokufa, na wewe kuwa hivyo hivyo, endelea kukua kwenye biashara yako, endelea kukua kwenye kazi yako na endelea kukua kwenye kipaji chako bila ya kujali ni umri gani unao.
Siku utakayojiona kwamba wewe ndio unajua kila kitu, wewe ndio unaweza kila siku, hii ndio siku ambayo unajilaani mwenyewe na unaanza kurudi nyuma na kushindwa kufikia mafanikio makubwa zaidi.
TAMKO LA LEO;
Kauli za enzi hizo ni kauli sumu kabisa kwangu kufikia mafanikio. Kuanzia sasa nitahakikisha kila siku nakuwa bora kuliko siku iliyopita. Sitaki nijisahau halafu nije kuona kwamba siku zilizopita nilikuwa vizuri. Nitajifunza kila siku, nitaweka juhudi kila siku na kila siku ya maisha yangu nitazidi kuwa bora kwenye kile ninachofanya. Najua hii ndio njia ya uhakika ya kufikia mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 169 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Tuesday, June 16, 2015

UKURASA WA 167; Maisha Ni Mchezo Na Sheria Za Kuushinda.

Kuna kauli nyingi sana kuhusu maisha. Mfano wa kauli hizo ni;
Maisha ni mapambano...
Maisha ni vita...
Maisha ni safari....
Na nyingine nyingi. Lakini leo nataka nikuambie kwamba katika kauli zote hizi kuhusu maisha, hakuna ambayo inayaelezea vizuri maisha. Na hapa tutajadili ile ambayo inayaelezea vizuri maisha yetu wanadamu.
Kauli inayoelezea maisha vizuri ni maisha ni mchezo. Ndio maisha ni mchezo na kama ilivyo michezo mingine kuna ambao wanashinda na kuna ambao wanashindwa. Na ili uweze kucheza vizuri mchezo wowote, kwanza kabisa lazima uzijue sheria za mchezo na uweze kuzitumia vizuri ili kushinda mchezo huo.
SOMA; BIASHARA LEO; Mtazamo Wa Kuvuna Na Mtazamo Wa Kujenga.
Maisha ni mchezo na katika mchezo huu kuna makundi mbalimbali ya watu. Kuna wale ambao ni wachezaji hasa ambao wapo uwanjani na wanacheza haswa, hawa ni wale ambao wanaishi maisha yao na wanayafurahia.
Pia kuna wale ambao ni washabiki, wanakaa nje ya uwanja na kuangalia mchezo. Hawa ni wale watu ambao hawana maisha yao wanayoishi, wao hufanya kile ambacho kila mtu anafanya. Watu hawa ni wazuri wa kukosoa wenzao, kama ambavyo mshabiki aliye nje ya uwanja anavyoweza kumkosoa mchezaji kwa urahisi.
Ili kushinda mchezo wowote kuna sheria muhimu unatakiwa kuzijua. Je unazijua sheria za kushinda huu mchezo wa maisha? Zipo wazi na hazina usumbufu. Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa makala hizi mpaka sasa unazijua vizuri sheria hizi. Leo nataka niongeze moja muhimu;
Sheria ya kwanza na muhimu kabisa itakayokuwezesha kushinda kwenye mchezo huu wa maisha ni kuendelea kuwepo kwenye mchezo. Haijalishi ni kitu gani kimetokea, haijalishi ni changamoto gani unayopitia, ili uweze kushinda mchezo huu ni lazima uendelee kuwa uwanjani na uendelee kucheza. Hivyo ndivyo ilivyo kwenye maisha, haijalishi nini kimetokea, haijalishi ni changamoto gani unapitia, maisha lazima yaendelee.
Ongeza sheria nyingine kumi kwenye hii moja ambazo umeshajifunza mpaka sasa. Ukipenda nitumie kwa email, utakuwa umejiwekea msingi mzuri wa kuzifuata.
TAMKO LA LEO;
Maisha ni mchezo na kama ilivyo michezo mingine yote, kuna sheria za mchezo huu. Sheria ya kwanza kabisa ya mchezo huu ni kwamba mchezo lazima uendelee hata kama kuna jambo baya kiasi gani limetokea. Maana ili uweze kushinda mchezo wowote ni lazima uwepo uwanjani na uweke juhudi na maarifa na nidhamu na uaminifu na......
Tukutane kwenye ukurasa wa 168 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Monday, June 15, 2015

UKURASA WA 166; Usijishike Na Vitu Hivi Kwenye Maisha Yako, Yatakuwa Magumu Sana.

Lengo la kila makala ninayoandika, lengo la kila ujumbe ninaoutoa wka njia mbali mbali iwe ni maongezi au hata video(angalia na jiunge na AMKA TV) ni kukupa wewe maarifa na mbinu za kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Kwa kuwa hiki ndio unachotaka kwenye maisha yako, au sio?
Leo nataka nikushirikishe baadhi ya vitu ambavyo usikubali kabisa kujishikiza navyo kwenye maisha. Kwa kujishikiza na vitu hivi unajiandaa kukatishwa tamaa na kuyafanya maisha yako kuwa magumu sana.
Tumewahi kujadili hapa kuhusiana na vitu tunavyokutana navyo kwenye maisha. Na tukasema kila kitu ulichanacho au unachokutana nacho kwenye maisha kinaingia katika moja ya makundi haya mawili. Kundi la kwanza ni vitu unavyoweza kuviathiri au kuvidhibiti na kundi la pili ni vitu ambavyo huwezi kuviathiri au kuvidhibiti.
Sasa leo nataka tujadili vitu ambavyo huwezi kuviathiri au kuvithibiti. Vitu unavyoweza kuviathiri tulishavijadili kwenye makala hii; Kitu Pekee Unachoweza Kukidhibiti Kwenye Maisha Yako.
Kwenye maisha yako usijishike na vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti, utajitengenezea nafasi kubwa ya kuumia moyo na kukatishwa tamaa. Huwezi kudhibiti ni kwa muda gani familia yako na marafiki zako wataishi. Huwezi kudhibiti ni kwamba utapandishwa cheo kazini au la. Huwezi kudhibiti kwamba kila biashara utakayofanya lazima ufanikiwe. Huwezi kudhibiti kama mwenza au mchuma uliyenaye mtakuwa pamoja mpaka kifo kiwatenganishe.
Hivi ni baadhi ya vitu vilivyopo nje ya uwezo wako wa udhibiti, japo unaweza kutengeneza mazingira mazuri na kuwa na vitu hivyo. Lengo la kujadili haya ni wewe kutouweka maisha yako yote katika vitu ambavyo huwezi kuvidhibiti. Kujua kwamba lolote linaweza kutokea ambalo lipo nje ya uwezo wako na likavuruga kila ambacho ulikuwa unaamini.
Hivyo furahia vitu kama vilivyo ila jua vinaweza kubadilika muda wowote bila ya wewe kutaarifiwa.
TAMKO LA LEO;
Najua kuna vitu vingi kwenye maisha siwezi kuvidhibiti. Kuanzia sasa sitoshikilia maisha yangu kwenye vitu hivi. Nitavifurahia wakati ninavyo na nitafanya juhudi zilizopo ndani ya uwezo wangu kuvikuza viwepo, ila pale vitakapoondoka kwa sababu ambazo siwezi kuzizuia nitajua ni sehemu ya maisha na sitokata tamaa na maisha yangu.
Tukutane kwenye ukurasa wa 167 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Sunday, June 14, 2015

UKURASA WA 165; Kuna Kitu Hujui? Hongera Sana Na Jua Jinsi Ya Kukitumia Hapa.

Moja ya sababu ambazo watu wamekuwa wakizitumia kwamba zinawazuia kufikia mafanikio ni kutokujua vitu fulani au kwa kuelewa zaidi kutokuwa na uzoefu. Kwa kuwa mimi lengo langu ni kukuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa, nahakikisha visababu hivi vinakosa nguvu na wewe unaanza kufanyia kazi kile unachotaka kupata.
Sasa leo tuanze na vitu ambavyo huvijui. Kama kuna vitu hujui, kama kuna vitu huna uzoefu navyo, kwanza hongera sana kwa sababu umedhibitisha kwamba wewe ni binadamu. Kila mtu alizaliwa akiwa anajua kitu kimoja kikubwa, jinsi ya ku “survive”, yaani jinsi ya kupona kwenye haya mazingira. Ndio maana mtoto hata akizaliwa leo, anajua kunyonya na kulia pia ili kufikisha ujumbe kwamba kuna kitu sio kizuri.
Lakini vitu vingine vyote kwenye maisha yako, ulizaliwa ukiwa hujui na sasa unajua. Je kuna maajabu hapa, la hasha, ulijifunza. Ulizaliwa hujui kusoma wala kuandika, ila sasa hivi upo hapa na unasoma makala hizi nzuri zinazokupatia maarifa. Ulizaliwa ukiwa hujui lugha yoyote zaidi ya kulia, la kwa sasa huenda unajua lugha sio chini ya tatu. Ulizaliwa ukiwa hujui kupika, kuendesha chombo cha usafiri na vingine vingi ambavyo kwa sasa unafanya, lakini uliweza kujifunza na sasa unavifanya.
Sasa kwa nini unatumia hicho unachoshindwa kufanya sasa kama kigezo cha wewe kuacha kufanya au kama sababu ya kushindwa? Si unaweza kujifunza kama ulivyojifunza hivyo vitu vingine?
SOMA; Umuhimu Na Jinsi Ya Kujenga Uaminifu Kwa Wateja Wako.
Kama kuna kitu chochote ambacho unafikiri kwa kutokukijua kinakuzuia kufikia mafanikio, jifunze kitu hicho. Tunaishi kwenye dunia ambayo kujifunza kumerahisishwa sana. Kwa kutumia simu yao tu unaweza kujifunza chochote unachotaka kujifunza. Tumia nafasi hii vizuri. Iwe unataka kujifunza upishi, iwe kujifunza uandishi, iwe kujifunza lugha ya kigeni, iwe kujifunza biashara na mengine mengi yanawezekana.
Wakati mwingine ukisema kwamba hujafikia mafanikio uliyotaka kwa sababu hujui kitu fulani utakuwa unatudanganya, maana ukweli ni kwamba ulikuwa na nafasi ya kujua ila hukuitumia vizuri. Anza sasa kuitumia nafasi hiyo.
TAMKO LA LEO;
Kitu chochote ambacho sikijui sio kikwazo kwangu kufikia mafanikio, bali hiki ni kitu muhimu ninachotakiwa kujifunza ili niweze kufikia mafanikio makubwa. Nitajifunza kila kitu muhimu ninachotakiwa kujua ili kufikia mafanikio, kama ambavyo nimejifunza vitu vingine kwenye maisha.
Tukutane kwenye ukurasa wa 166 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Saturday, June 13, 2015

UKURASA WA 164; Vitu Ambavyo Ni Rahisi Kufanya.... Na Madhara Yake.

Vitu ambavyo ni rahisi kufanya ndio vitu ambavyo havina thamani kubwa kwako. N vitu ambavyo hutakiwi kuviamini au kuvitegemea maana havitakupeleka kule ambapo unataka kufika.
Unapokutana na changamoto yoyote kuna njia mbili za kufuata, kupambana na changamoto hiyo, kitu ambacho ni kigumu kufanya na kinaweza kukuletea changamoto zaidi. Au unaweza kuikimbia changamoto hiyo kitu ambacho ni rahisi kufanya.
Kitu ambacho ni kigumu kufanya, kupambana na changamoto hiyo sasa kina nafasi kubwa ya kukuletea mafanikio. Lakini kitu ambacho ni rahisi kufanya, kukimbia changamoto hiyo kwa kulalamika au kuikataa kama vile haipo au haikuhusu hakuwezi kukuletea mafanikio kabisa. Kitu cha uhakika unachokuwa nacho ni kwamba kitu rahisi kufanya kitakupeleka kwenye matatizo zaidi.
SOMA; BIASHARA LEO; Kutojali Kwako Kunavyokuletea Hasara Kwenye Biashara.
Kwenye maisha, kazi na hata biashara, kitu ambacho ni rahisi kufanya hakiwezi kukuletea mafanikio makubwa na mara nyingi kitakuingiza kwenye matatizo zaidi
Baadhi ya vitu ambavyo ni rahisi kufanya na unatakiwa kuviepuka;
1. Kuongea sana badala ya kutenda.
2. Kukosoa.
3. Kutumia ulevi ili kuondokana na tatizo.
4. Kulaumu wengine.
5. Umbeya, masengenyo na majungu.
6. Kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.
7. Kulala sana.
8. Kusema NDIO kwa kila jambo.
9. Kusema uongo.
10. Kuiba au kudhulumu wengine.
Acha mara moja kufanya vitu hivi ambavyo unaona ni rahisi lakini ndio vinazidi kukurudisha nyuma.
TAMKO LA LEO;
Vitu ambavyo ni rahisi kufanya ndio vimekuwa vinanizuia mimi kusonga mbele na kufikia mafanikio. Vitu hivi vimekuwa vinaniweka mbali zaidi na mafanikio na wakati mwingine kuniingiza kwenye matatizo makubwa zaidi. Kuanzia sasa nitaacha kukimbilia kufanya vitu ambavyo ni rahisi na kukabiliana na vile vigumu kwa sababu najua ndio vitakavyoniletea mafanikio.
Tukutane kwenye ukurasa wa 165 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Friday, June 12, 2015

UKURASA WA 163; Unapokuwa Mpinzani Wako Mwenyewe... Na Hasara Yake Kwenye Maisha Yako.

Moja ya changamoto kubwa zinazowazuia watu wengi kupata kile wanachotaka, kufikia mafanikio wanayotarajia ni kuwa wapinzani wao wenyewe. Yaani wewe unakuwa mpinzani wako mwenyewe. Bado hujaelewa inakuwaje? Nitakufafanulia vizuri zaidi ili uweze kuelewa na kuchukua hatua pia.
Umekuwa unajifunza mambo mazuri na yatakayobadili maisha yako na unakubali kabisa ya kwamba utakwenda kufanyia kazi yale ambayo umejifunza. Ila unapoanza kuyafanyia kazi yale uliyojifunza yanaanza kukujia mawazo kwamba unachofanya sio sahihi au hakiwezi kukuletea kile unachotaka.
Labda umejifunza kuhusu kuamka asubuhi na mapema ili ufanye mambo yako ukiwa na utulivu. Unaamka siku ya kwanza na ya pili baada unaanza kufikiria kwa nini nijitese, au ina maana gani, acha niendelee na muda wangu wa kawaida wa kuamka.
Au umejifunza kutolalamika au kulaumu mtu yeyote yule, iwe ndugu, serikali, bosi, bali wewe ni kuchukua hatua. Baadae unaona haiwezekani, hawa watu ni lazima walaumiwe, wanafanya mambo ambayo sio. Unawalaumu, unaridhika na maisha yako yanaendelea kuwa kama yalivyokuwa zamani.
SOMA; Naomba Ufanye Changamoto Hii Ya Siku Kumi, Utabadili Sana Maisha Yako.
Leo nikuambie kitu kimoja kwamba kuwa adui yako mwenyewe ni kikwazo namba moja kwako kubadili maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Unaweza kuwa na mawazo mazuri sana, unaweza kuwa na mipango mizuri sana ila kama hutaacha kuwa adui yako mwenyewe, kama hutaacha kuwa mpinzani wako mwenyewe hakuna kitakachobadilika kwenye maisha yako.
Safari ya kubadili maisha yako na kufikia mafanikio sio rahisi kama unavyofikiri. Utapata upinzani mkubwa kuanzia ndani yako mwenyewe na hata kwa wale wanaokuzunguka. Ukishafanya maamuzi ya kubadili maisha yako, komaa nayo na usirudi tena nyuma, hata kama utajipa sababu nzuri kiasi gani.
TAMKO LA LEO;
Najua mara nyingi nimekuwa mpinzani wangu mwenyewe. Nimekuwa napanga kubadili maisha yangu ili kufikia mafanikio lakini mimi mwenyewe naanza kupinga vile nilivyopanga kufanya. Kuanzia leo naondoa kabisa upinzani mkubwa ambao nimekuwa najiwekea mwenyewe. Nikishapanga kitu nitakomaa nacho mpaka mwisho, mpaka nione kile ninachotarajia kuona.
Tukutane kwenye ukurasa wa 164 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.
Kuhakikisha hukosi mfululizo huu wa makala za KURASA 365 bonyeza hapa na uweke email.
Kusoma makala zilizopita za KURASA 365 ZA MWAKA 2015 bonyeza hayo maandishi.
Pia washirikishe wengine makala hii kwa kubonyeza vitufe vya facebook au twitter hapo chini. Pia watumie makala hii nzuri kwa njia ya email.
Kwa lolote andika email kwenda makirita@kisimachamaarifa.co.tz
Kujifunza zaidi ili kuweza kufikia mafanikio makubwa jiunge na KISIMA CHA MAARIFA bonyeza hayo maandishi kupata utaratibu.
TUPO PAMOJA.

Thursday, June 11, 2015

UKURASA WA 162; Hakuna Namna Nyingine...

Hakuna namna nyingine, ni lazima ufanikiwe.
Kuna watu ambao wameanzia chini kuliko ulikoanzia wewe lakini wameweza kufanikiwa, kwa nini na wewe usifanikiwe?
Kuna watu ambao wamepata elimu ndogo kuliko uliyopata wewe, lakini wameweza kufanya mambo makubwa kwenye maisha yako, kwa nini wewe ushindwe kufanya?
Kuna watu ambao walikataliwa na kutelekezwa. Lakini hawakujali hilo, waliendelea na kile kilichokuwa ndani yao na sasa wako mbali, kwa nini na wewe usiende mbali zaidi ya ulipofika sasa?
Siandiki haya kukulinganisha wewe na wengine, au kukufanya ujilaumu kwa nini ushindwe na waliokuwa chini zaidi yako.
Ila naandika haya kukumbia kwa hapo ulipofikia sasa hakuna namna nyingine bali ni kufanikiwa tu. Hakuna uchawi utakaokuletea mafanikio haya, hakuna serikali itakayokuletea mafanikio haya, hakuna ndugu atakayekuletea mafanikio haya.
Amka sasa na uanze kupigania kile kilicho chako, amka cha kulalamika, weka juhudi kwenye kazi yako, wenzako wakienda kupiga soga wewe fanya kazi, wenzako wakipitia viti virefu jioni wewe jiandae na kazi, kidogo kidogo na wewe utachomoza na utakuwa habari ya mjini.
Acha kuishia kusema fulani alianzia hapa kafika pale, ingia kwenye kazi na wewe uwe sehemu ya hadithi nzuri kwa wengine.

TAMKO LA LEO;
Leo hii nimeamua kwamba hakuna namna nyingine ila kufikia mafanikio kwenye maisha yangu. Najua uwezo ninao na hivyo naweka juhudi kutengeneza mafanikio makubwa.

Tukutane kwenye ukurasa wa 163 kesho, Like page yangu ya Coach Makirita Amani uendelee kupata mambo mazuri ya kuboresha kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla.