Jiunge Hapa Kupata Makala Mpya Inapotoka!

We'll not spam mate! We promise.

Sunday, November 30, 2014

Kesho ni siku muhimu sana kwako, na itumie kufanya jambo hili moja muhimu.

Kesho ni tarehe moja mwezi wa kumi na mbili. Maana yake ni kwamba ni siku ya kwanza ya mwezi wa mwisho wa mwaka huu 2014.
Kuanzia kesho zitakuwa zimebaki siku 30 tu mwaka uishe!
Je mwaka huu 2014 uliendaje kwako?
Je malengo na mipango uliyojiwekea umeyatimiza!
Tumia siku ya kesho kutafakari mwaka huu umekwendaje.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.

Sheria Kumi Za Familia Za Kuzingatia

NENO LA LEO; Uwekezaji Unaolipa Riba Kubwa Sana

An investment in knowledge pays the best interest. –Benjamin Franklin

Uwekezaji kwenye elimu/ujuzi ndio uwekezaji unaolipa riba kubwa sana.

Anza sasa kuwekeza kwenye ujuzi na elimu yako, jifunze mambo mapya na yafanyie kazi.

Jinsi unavyojifunza zaidi ndivyo unavyoongeza thamani yako na hivyo kuongeza kipato chako.

Nakutakia siku njema.

Saturday, November 29, 2014

UMUHIMU WA KUSOMA ZAIDI NA KUSOMA KILA MARA;

i. Jinsi unavyoishi jifunze jinsi ya kuishi, hakuna anayejua kila kitu.
ii. Viongozi bora wa uchumi mpya watakuwa ni wale wanaoweza kufikiri vizuri.
iii. Kufikiri vizuri kunajengwa na kusoma sana.
iv. Unachohitaji ili kubadili maisha yako moja kwa moja ni wazo moja tu kutoka kwenye kitabu sahihi.
v. Beba kitabu popote unapokuwa, ukiwa unamsubiri mtu soma, ukiwa kwenye foleni soma. Usipoteze muda wako kulalamika.
vi. Kama hujasoma kitu kizuri leo, hujaishi siku ya leo. Na kusoma huku sio habari, bali kitu kinachoweza kukusogeza karibu na malengo yako kweny maisha.
Kupata nafasi ya kusoma zaidi tembelea www.voraciousreaderstz.blogspot.com

Mambo matatu yatakayokufanya uishi maisha marefu.

Magonjwa mengi yanayowafanya watu kufa wakiwa na umri mdogo yanatokana na mtindo wa maisha tunaochagua.
Magonjwa kama presha ya juu, kisukari na hata kansa yanatokana na mitindo mbalimbali ya maisha.
Hapa nakushirikisha mambo matatu unayoweza kuanza kuyafanya leo na ukapunguza nafasi ya wewe kupata magonjwa haya na hivyo kuishi miaka mirefu.
1. Kula vizuri.
Naposema kula vizuri namaanisha ule mlo kamili. Kula mafita kidogo na kwa mtu mzima kula wanga kidogo. Kula matunda na mboga ,boga kwa wingi na pia kunywa maji mengi.
2. Fanya mazoezi.
Mazoezi ni muhimu sana kwa afya yako. Na mazoezi sio lazima ulipie gym au kukimbia barabarani japo hiyo ni sehemu nzuri ya mazoezi.
Unaweza kuchagua kutembea kwa miguu badala ya kupanda gari, kupanda ngazi badala ya kupanda lifti na kusimama na kufuata kitu mwenyewe badala ya kuagiza uletewe.
3. Usivute sigara.
Kila unapovuta sigara moja unapunguza dakika 14 za maisha yako. Sigara ina kemikali zaidi ya elfu moja zinazosababisha kansa. Karibu kila kansa inayompata binadamu inaweza kuchochewa na uvutaji wa sigara.
Na sigara sio lazima uvute wewe, hata ule moshi unaovuta kutoka kwa watu wanaovuta sigara una athari kubwa kwa afya yako.
Hayo ndio mambo matatu ambayo unaweza kuanza kuyafanya leo na ukaboresha afya yako na kyongeza siku zako za kuishi.
Nakutakia kila la kheri,
TUPO PAMOJA.
www.kisimachamaarifa.co.tz
www.amkamtanzania.com

NENO LA LEO; Siku Mbili Muhimu Sana Kwenye Maisha Yako.

The two most important days in your life are the day you are born and the day you find out why. –Mark Twain

Siku mbili muhimu sana kwenye maisha yako ni siku uliyozaliwa na siku uliyojua kwa nini ulizaliwa.

Najua wengi tunajua siku tulizozaliwa ila ni wachache sana wanaojua kwa nini walizaliwa.

Kama bado hujajua kwa nini ulizaliwa kwaribu tusaidiane kujua kwa nini ulizaliwa, yaani ni nini hasa unatakiwa kufanya na maisha yako.

Andika email yenye kichwa cha habari KWA NINI NILIZALIWA na maelezo mengine muhimu kuhusu wewe kisha tuma kwenye email ushauri@kisimachamaarifa.co.tz

Nakutakia siku njema.

Friday, November 28, 2014

NENO LA LEO; Kuhusu Kuendesha Siku Au Kuendeshwa na Siku.

Either you run the day, or the day runs you. –Jim Rohn

Kwenye siku yako ni labda unaiendesha siku au siku inakuendesha wewe.

Unaiendesha siku pale ambapo unakuwa na malengo na mipango yako ambayo unaifuata.

Unaendeshwa na siku pale ambapo unafanya kile kinachotokea mbele yako.

NINAJUA UNAJUA UNACHOTAKIWA KUFANYA, FANYA SASA, LEO HII ILI UWEZE KUIENDESHA SIKU YAKO.

Nakutakia siku njema.

Thursday, November 27, 2014

NENO LA LEO; Unachohitaji Ili Kubadili Maisha Yako.

You can never cross the ocean until you have the courage to lose sight of the shore. –Christopher Columbus

Huwezi kuivuka bahari mpaka pale utakapokuwa na ujasiri wa kupoteza taswira ya ufukwe.

Tunapenda vitu vizuri lakini tunaogopa kupoteza tulivyo navyo. Huwezi kupata vitu vipya kama hutaacha hivyo ulivyonavyo sasa.

Nakutakia siku njema.

Wednesday, November 26, 2014

NENO LA LEO; MUDA MZURI WA KUPAMDA MTI.

The best time to plant a tree was 20 years ago. The second best time is now.

Muda mzuri wa kupanda mti ilikuwa miaka 20 iliyopita. Muda mwingine mzuri ni sasa.

Kila kitu kinahitaji maandalizi ya muda mrefu. Hivyo ili kuwa na maisha bora baadae inabidi uanze kufanya mabadiliko sasa.

Nakutakia siku njema.

Tuesday, November 25, 2014

NENO LA LEO; FURSA UNAZOZIKOSA.

You miss 100% of the shots you don’t take. –Wayne Gretzky

Unakosa asilimia 100 ya fursa ambazo hujazichukulia hatua.

Acha kuendelea kusita sita, unapoteza fursa nyingi na muda wako pia.

Wakati wa kuchukua hatua ni sasa.

Nakutakia siku njema.

Monday, November 24, 2014

Hivi ndivyo shauku inavyokufanya kuwa mteja bila ya kupenda.

Sasa hivi tumekuwa watu wa kuendeshwa na shauku inayotokana na hisia. Na hii imetufanya tuwe wateja kwa wanaoweza kuzitumia hisia na shauku zetu.
Kwa mfano;
Kuna tofauti gani kwa anayenunua simu mpya iliyotoka leo kwa kusubiria muda mrefu na atakayekuja kuinunua kesho wakati kumetulia?
Kuna tofauti gani kati ya anayesikia habari mpya leo, BREAKING NEWS na atakayeisikia kesho?
Kuna tofauti gani kwa atakayekuwa wa kwanza kusambaza habari na ambae hatakuwa na haraka hiyo?
Yote haya na mengine mengi hayana tofauti ila yanatufanya tuwe wateja wa matoleo mapya, habari zilizovunjika na mbaya zaidi kusambaza habari ambazo hatuna uhakika nazo ili tu uwe wa kwanza......
Huna haja ya kuwa wa kwanza katika mambo haya, ni kujiongezea tu msongo.

NENO LA LEO; Kuhusu Fedha Kutonunua Furaha.

Watu wote wanaosema fedha haiwezi kununua furaha nao hawana fedha za kuwatosha. Sijawahi kumsikia tajiri akitumia kauli hiyo kwamba fedha haiwezi kununua furaha.

Hivyo basi badala ya kukubali tu kauli hiyo kwa nini usiifanyie majaribio? Kuwa na fedha nyingi halafu uone kama kweli zinaweza kununua furaha au la.

Nakutakia siku njema.

Sunday, November 23, 2014

Mahitaji Manne Ya Mtu Kuwa Kiongozi.

Ili uweze kuwa kiongozi bora na mwenye mafanikio kuna vitu vinne unavyotakiwa kuwa navyo na uweze kuvisimamia. Kwa kujua na kusimamia vitu hivi kutakuwezesha kufanikiwa sana kama kiongozi.

1. Kuweza kujisimamia mwenyewe.

Kiongozi bora ni yule ambaye anayeweza kujisimamia mwenyewe. Ni lazima uweze kujiwekea malengo na mipango yako mwenyewe na uweze kuifuata bila ya kusimamiwa na mtu mwingine yeyote. Kama unahitaji kusimamiwa ndio uweze kutekeleza majukumu yako basi wewe sio kiongozi bali ni mfuasi. Na kama ukijaribu kuongoza kama unakosa tabia ya kujisimamia mwenyewe utashindwa vibaya sana.

2. Kuweza kutatua matatizo.

Kazi kubwa ya kiongozi ni moja, kutatua matatizo. Ili uweze kuwa kiongozi bora inabidi uweze kuyaangalia matatizo kwa jinsi gani yanaweza kutatuliwa. Kama unaogopeshwa na tatizo na kuona haliwezi kutatuliwa wewe sio kiongozi. Kila tatizo lina utatuzi wake. Ni kazi yako kama kiongozi kuja na njia za kutatua tatizo hilo na hivyo kuboresha hali iliyopo.

3. Kuweza kufanya mawasiliano mazuri.

Kiongozi bora ni yule ambaye anaweza kufikia ujumbe wake kwa watu anaowaongoza na wakauelewa na kuufanyia kazi ujumbe huo. Ili kuweza kufikisha ujumbe wao vizuri ni lazima uwe na mbinu nzuri za mawasiliano. Mawasiliano yanaweza kuwa ya maneno, maandishi au hata vitendo. Jinsi ambavyo unawasilisha ujumbe wako unaweza kuwa na ushawishi mkubwa au ukapuuzwa na wale wanaoupokea. Ni muhimu kujifunza mbinu bora za kufanya mawasiliano ili uweze kufikisha ujumbe wako na ufanyiwe kazi.

4. Kuweza kujenga mahusiano.

Kiongozi ni mtu na anayewaongoza ni watu. Ili uweze kuwa kiongozi bora ni lazima uwe na mahusiano mazuri na wale ambao unawaongoza. Kiongozi sio mtawala kwamba anachokisema yeye ndio mwisho, bali anahitaji kujenga urafiki na watu ambao anawaongoza. Kwa urafiki huu watu anaowaongoza watakuwa tayari kumshauri mambo mengi ambayo yatamsaidia kuongoza vizuri zaidi.

Hayo ndio mambo manne unayohitaji kuwa nayo ili kuwa kiongozi bora. Habari nzuri ni kwamba mambo yote hayo manne unaweza kujifunza na kuyaendeleza kwenye uongozi wako.

Nakutakia kila la kheri kwenye mafanikio yako kama kiongozi.

TUPO PAMOJA.

Saturday, November 22, 2014

NENO LA LEO; Tofauti Ya Washindi Na Washindwa.

Winners make goals... losers make excuses!

Washindi wanatengeneza malengo, washindwa wanatengeneza visingizio.

Amua leo kuwa mshindi na weka malengo na mipango mikubwa kwenye maisha yako. Acha sasa kutafuta visingizio.

Nakutakia siku njema.

Thursday, November 20, 2014

NENO LA LEO; Kuhusu Kujitetea.

It will do no good to argue if you're in the wrong. If you're right, you don't need to.

Kama umekosea au uko upande ambao sio sahihi, kujitetea hakuwezi kusaidia. Kama uko sahihi huna haja ya kujitetea.

Nakutakia siku njema.

Tuesday, November 18, 2014

NENO LA LEO; Mwalimu Bora.

The best teachers teach from the heart, not from the
book.

Mwalimu bora anafundisha kutoka moyoni na sio kutoka kwenye vitabu.

Nakutakia siku njema.

Monday, November 17, 2014

Hivi ndivyo unavyoweza kuianza wiki yenye mafanikio.

Habari za asubuhi rafiki?
Ni siku nyingine mpya na mwanzo wa wiki mpya.
Naamini umeipangilia wiki yako vizuri kwa ajili ya kufikia mafanikio makubwa.
Wiki hii fanya kitu hiki kimoja;
Dhibiti kiwango cha taarifa unazopata, hasa kupitia vyombo vya habari. Hii ni kwa sababu taarifa nyingi ni;
i. Zinakula muda wako mwingi
ii. Ni hasi
iii. Hazina uhusiano na malengo yako.
iv. Huwezi kuziathiri, ziko nje ya uwezo wako.
Nakutakia wiki njema na yenye mafanikio makubwa.
TUPO PAMOJA.
Tembelea www.amkaconsultants.blogspot.com kujifunza zaidi.

Saturday, November 15, 2014

NENO LA LEO; Kuhusu Kuamini Uongo.

It is easier to believe a lie that you have heard a
thousand times, than the truth that you have only heard once.

Ni rahisi kuamini uongo uliousikia mara elfu moja kuliko kuamini ukweli uliousikia mara moja.

Ukweli utabaki kuwa ukweli, ukatae au ukubali.

Nakutakia siku njema.

Friday, November 14, 2014

NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Machozi

Tears are words the heart can't express.

Machozi ni maneno ambayo moyo hauwezi kuyaeleza.

Machozi ni hisia kubwa sana inayotolewa na mtu, inaweza kuwa furaha au inaweza kuwa huzuni. Hakikisha unaleta machozi ya furaha kwa watu wako wa karibu.

Nakutakia siku njema.

Wednesday, November 12, 2014

NENO LA LEO; Chanzo Cha Mafanikio.

Achieving starts with believing in yourself.

Mafanikio huanza pale unapojiamini mwenyewe.

Anza sasa kujiamini na amini una uwezo mkubwa ulioko ndani yako wa kufikia mafanikio makubwa.

Nakutakia siku njema.

Tuesday, November 11, 2014

NENO LA LEO; Mambo Unayotakiwa Kufanya.

You have to do what others won't. To achieve what others don't.

Unatakiwa kufanya mambo ambayo watu wengine hawafanyi ili kupata vitu ambavyo wengine hawapati.

Kupata mafanikio makubwa unahitaji kuwa tofauti na wengine.

Nakutakia siku njema.

Monday, November 10, 2014

NENO LA LEO; Kuhusu Mtu Anayejua Kila Kitu.

Any man who knows all the answers most likely misunderstood the questions.

Mtu anayejua majibu yote kuna uwezekano mkubwa haelewi maswali.

Katika ulimwengu wa sasa ni vigumu sana kujua kila kitu, chagua vitu vichache unavyotaka kuvijua na vijue vizuri.

Nakutakia siku njema.

Sunday, November 9, 2014

Mambo 21 muhimu ya kiufanya kila siku ili kuwa na maisha yenye mafanikio.

HABARI ZA LEO RAFIKI?
Naomba nikushirikishe Vitu 21 rahisi vya kufanya kila siku ili kuwa na maisha yenye furaha na mafanikio.
i. Lala masaa nane kwa siku.
ii. Kula milo miwili kwa siku.
iii. Usiangalie TV
iv. Usile vyakula vya haraka
v. Usilaumu wala kulalamika
vi. Usisengenye, usishiriki majungu na umbea.
vii. Onesha shukrani kwa marafiki.
viii. Andika orodha ya mawazo bora kila siku.
ix. Iambie nafsi yako unapoamka kwamba utakwenda kusaidia na kuokoa maisha ya watu kwa siku hiyo.
x. Andika mambo unayopanga kufanya kwa siku.
xi. Mshangaze mtu.
xii. Fikiria watu kumi ambao unashukuru kuwa nao kwenye maisha yako.
xiii. Msamehe mtu.
xiv. Panda ngazi badala ya lifti.
xv. Usiseme ndio wakati unafikiria kusema hapana.
xvi. Mwambie mtu kila siku kwamba unampenda.
xvii. Soma sura moja ya kitabu cha mtu anayekuhamasisha.
xviii. Weka mipango ya kutumia muda na rafiki yako.
xix. Pumua kwa kina na taratibu.
xx. Jifunze kitu kipya kila siku, pata walau saa moja ya kujisomea.
xxi. Fikiria watu wawili unaoweza kuwakutanisha na wakasaidiana na kushirikiana.
Kutoka kwa James Altucher - Choose Yourself.
Tembelea www.amkaconsultants.blogspot.com kujifunza zaidi.
TUPO PAMOJA, TUTAKUTANA KILELENI.

Nguzo Kuu Ya Uongozi; Tekeleza Kile Unachoahidi.

Katika kujijenga kuwa kiongozi bora na imara kuna misingi mingi ya uongozi ambayo unatakiwa kuifuata. Kushindwa kufuata misingi hii kutapelekea uongozi wako kushindwa na hata kudharaulika sana.

Moja ya nguzo muhimu za uongozi ni kutekeleza kile unachoahidi. Kuongea ni rahisi sana na hivyo watu wengi hujikuta wakiongea mambo ambayo hawana uhakika kama wanaweza kuyatekeleza. Kwa kuwa kuongea ni rahisi watu hutumia nafasi hii kuongea mambo ambayo yatawafanya waonekane ni viongozi wazuri ila hawana uwezo wa kuyatekeleza.

Madhara ya kuahidi mambo usiyoweza kutekeleza.

1. Inakuondolea uaminifu.

Unapoahidi mambo halafu ukashindwa kuyatekeleza watu huondoa uaminifu kwako. Hivyo wakati mwingine utakapowaahidi hawatakusikiliza na hata wakikusikiliza hawataweka maanani uliyowaambia. Kwa sababu binadamu wana tabia moja kwamba ukishamdanganya mtu mara moja kila wakati atakuwa na wasi wasi na wewe.

2. Itakuondolea ushawishi.

Uongozi ni ushawishi, kama utaahidi mambo ambayo huwezi kuyatekeleza na kufanikiwakuwashawishi watu mara ya kwanza, baadae utapoteza ushawishi huo kama hukutekeleza yale uliyoahidi mara ya kwanza. Unapopoteza ushawishi unapoteza uongozi.

3. Unapoteza heshima yako.

Unapokuwa mtu wa kutekeleza maneno yako unaheshimika na wale unaowaongoza na hata jamii kwa ujumla. Unapoanza kuahidi mambo ambayo unashindwa kuyatekeleza unapoteza heshima yako.

Anza sasa kutekeleza kile unachoahidi kufanya, itakujengea sifa nzuri kama kiongozi na itakuongezea ushawishi na heshima mbele ya jamii.

Kama umeahidi wateja kwamba utawapatia bidhaa au huduma bora tekeleza ahadi yako.

Kama umewaahidi wafanyakazi wako kwamba wakifikia kiwango fulani cha uzalishaji utawaongeza mshahara basi timiza ahadi yako wanapofikia kiwango hiko.

Kama umewaahidi wananchi wakupigie kura ili uweze kuwasaidia kufikia maendeleo, tekeleza ahadi uliyotoa.

Hivi ndivyo unavyoweza kuwa kiongozi bora, TEKELEZA AHADI ZAKO NA IKIWEZEKANA ONGEZA ZAIDI.

Nakutakia kila la kheri katika uongozi wako.

TUPO PAMOJA.

Saturday, November 8, 2014

NENO LA LEO; Kuhusu Kikomo Cha Kasi Kwenye Njia Ya Mafanikio.

There are no speed limits on the road to excellence.

Hakuna kikomo cha kazi kwenye njia ya mafanikio.

Amua leo kwenda kwa kasi kubwa ili uweze kufikia mafanikio makubwa. Hakuna mda wa kupoteza.

Nakutakia siku njema.

Friday, November 7, 2014

NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Msamaha

Forgiveness is all about me giving up my right to hurt you for hurting me.

Msamaha ni pale ambapo mimi naamua kupoteza haki yangu ya kukuumiza wewe kwa kuniumiza mimi.

Unaposamehe unaepuka kutengeneza maumivu zaidi.

Amua leo kuwasamehe wote waliokuumiza, maana kuendelea kukaa na kinyongo unazidi kuumia wewe.

Nakutakia siku njema.

Thursday, November 6, 2014

NENO LA LEO; Mambo Mawili Muhimu Sana Kujua Kuhusu Maisha.

Life can either be accepted or changed. If it is not
accepted, it must be changed. If it cannot be changed, then it must be accepted.

Maisha yanaweza kukubaliwa au yanaweza kubadilishwa. Kama hayakubaliwi ni lazima yabadilishwe. Kama hayawezi kubadilishwa ni lazima yakubaliwe.

Usiendelee tena kuteseka na maisha yako, kama kuna kitu hukipendi kibadilishe na kama huwezi kukibadilisha kikubali. Ukiweza kufanya hivi maisha yako yatakuwa ya furaha.

Nakutakia siku njema.

Wednesday, November 5, 2014

NENO LA LEO; Kukolea Kwenye Tabia Mbaya.

Bad habits are like a comfortable bed; they are easy to get into, but hard to get out of.

Tabia mbaya ni kama kitanda kizuri, ni rahisi kuingia ila ni vigumu sana kutoka.

Kama kuna tabia ambayo huipendi fanya jitihada kubwa kuondokana nayo.

Nakutakia siku njema.

Tuesday, November 4, 2014

NENO LA LEO; Mbinu Ya Kufikia Urefu Mkubwa.

To reach a great height a person needs to have great depth.

Kufikia urefu mkubwa mtu anahitaji kuwa na kina kikubwa.

Kiendacho juu kinategemea uimara wa kilichopo chini. Kama ilivyo kwamba ghorofa ndefu ina kina kikubwa na msingi imara.

Nakutakia siku njema.

Monday, November 3, 2014

Tukemee Tabia Hii Mbaya Kama Taifa.

Jana tarehe 02/11/2014 kulikuwa na mdahalo wa katiba ulioandaliwa na taasisi ya Mwalimu Nyerere uliokuwa unafanyika katika ukumbi wa ukumbi wa ubungo plaza.

Katika mdahalo huo waliokuwa wajumbe wa iliyokuwa tume ya katiba walialikwa kuzungumza na baadae wananchi waliohudhuria nao wangepata nafasi ya kuzungumzia katiba pendekezwa.

Lengo kubwa la mdahalo huo na mingine ambayo tuliahidiwa itafuata ilikuwa kuwapa uelewa wananchi juu ya katiba pendekezwa kabla wakati wa kupiga kura haujafika.

Binafsi ninaona kitu hiki ni kizuri sana maana taasisi inayoandaa midahalo hii haina uegemeo wowote wa kisiasa na hivyo itatoa nafasi nzuri ya wananchi kujifunza yaliyomo kwenye katiba pendekezwa.

Katika hali ya kushangaza wakati mdahalo unaendelea na Jaji Warioba akizungumza kiliibuka kikundi cha watu ambao walionesha mabango ya kupinga mdahalo ule na kusema kwamba wanaikubali katiba pendekezwa. Hata walipotakiwa kutulia chini ili mdahalo uweze kuendelea bado hawakusikia na hatimaye ikapelekea vurugu kubwa na mdahalo kuahirishwa.

WARIOBA

Kwanza kabisa hiki ni kitendo cha ajabu sana ambacho kinatakiw akulaaniwa na kila Mtanzania ambaye ana mapenzi mema na nchi hii. Ni kweli kabisa hatuwezi kukubaliana wote, ila kutofautiana kwetu kifikra na kihoja kusifanye tuonanae kama maadui. Hizi ni siasa chafu na za kitoto sana ambazo naona zinanyamaziwa na wanaofanya ujinga huu wanaonekana kama wanaleta manufaa kwa kikundi fulani.

Kama unaona mtu anakushinda kwa hoja njia sahihi ni kuleta fujo na kupigana? Hapana hii sio njia sahihi kabisa na kama tutaendelea kuacha mambo haya yaendelee tutalipeleka taifa kubaya.

Katiba ni kitu ambacho kinamhusu kila mwananchi na hivyo kila mwananchi ana uhuru wa kutoa maoni yake na hisia zake juu ya katiba hii. Lakini katika kutoa maoni hayo na hisia hizo usiingilie uhuru wa mwenzako au kuleta fujo au kumwona anayeamini tofauti na wewe ni adui.

Naomba watanzania wote tulaani kitendo hiki kilichotokea na tusitoe tena nafasi ya kutokea kwa kitendo kama hiki.

Tanzania ni nchi yetu sote, tushirikiane kuijenga.

TUPO PAMOJA.

LEO KATIKA HISTORIA; TAREHE 03/11/2014

November 3

1493
Christopher Columbus arrives at the Caribbee Isles (Dominica) during his second expedition.

1507
Leonardo da Vinci is commissioned to paint Lisa Gherardini ("Mona Lisa").

1529
The first parliament for five years opens in England and the Commons put forward bills against abuses amongst the clergy and in the church courts.

1794
Thomas Paine is released from a Parisian jail with help from the American ambassador James Monroe. He was arrested for having offended the Robespierre faction.

1813
American troops destroy the Indian village of Tallushatchee in the Mississippi Valley.

1868
Ulysses S. Grant elected the 18th president of the United States.

1883
A poorly trained Egyptian army, led by British General William Hicks, marches toward El Obeid in the Sudan–straight into a Mahdist ambush and massacre.

1883
The U.S. Supreme Court declares American Indians to be "dependent aliens."

1892
First automatic telephone exchange goes into operation in La Porte, Indiana.

1896
William McKinley is elected 25th president of the United States.

1912
The first all-metal plane flies near Issy, France, piloted by Ponche and Prinard.

1918
The German fleet at Kiel mutinies. This is the first act leading to Germany's capitulation in World War I.

1921
Milk drivers on strike dump thousands of gallons of milk onto New York City's streets.

1935
Left-wing groups in France form the Socialist and Republican Union.

1957
The Soviet Union launches Sputnik II with the dog Laika, the first animal in space, aboard.

1964
For the first time residents of Washington, D.C., are allowed to vote in a presidential election.

1964
Lyndon B. Johnson is elected the 36th president of the United States.

1964
Robert Kennedy, brother of the slain president, is elected as a senator from New York.

1967
The Battle of Dak To begins in Vietnam's Central Highlands; actually a series of engagements, the battle would continue through Nov. 22.

1969
US President Richard Nixon, speaking on TV and radio, asks the "silent majority" of the American people to support his policies and the continuing war effort in Vietnam.

1973
NASA launches Mariner 10, which will become the first probe to reach Mercury.

1979
Ku Klux Klansmen and neo-Nazis kill 5 and wound 7 members of the Communist Workers Party during a "Death to the Klan" rally in Greensboro, NC; the incident becomes known as the Greensboro Massacre.

1983
Jesse Jackson announces his candidacy for the office of president of the United States.

1986
The Lebanese magazine Ash-Shiraa reports the US has secretly been selling weapons to Iran in order to secure the release of 7 American hostages being held by pro-Iranian groups in Lebanon.

1992
Arkansas Governor Bill (William Jefferson) Clinton is elected 42nd president of the United States.

1997
US imposes economic sanctions against Sudan in response to human rights abuses and support of Islamic extremist groups.

Born on November 3

1718
John Montague, fourth Earl of Sandwich and inventor of the sandwich.

1794
William Cullen Bryant, poet and journalist.

1801
Karl Baedeker, German publisher, well known for travel guides.

1831
Ignatius Donnelly, American social reformer best known for his book Atlantis: The Antediluvian World.

1901
Andre Malraux, French novelist (Man's Fate).

1903
Walker Evans, photographer.

1909
James "Scotty" Reston, New York Times reporter, editor and columnist.

1918
Russell Long, U.S. senator from Louisiana from 1951 to 1968 and son of Huey P. Long.

1920
Oodgeroo Noonuccal [Kath Walker], Australian Aboriginal poet.

1933
Jeremy Brett, actor; best known for his portrayal of Sherlock Holmes in the Granada TV productions of Sir Arthur Conan Doyle's stories about the detective.

1933
Michael Dukakis, politician; the longest-serving governor in the history of the State of Massachusetts (1975-79, 1983-91); unsuccessful Democratic candidate for US presidency (1988).

1933
Amartya Sen, Indian economist, winner of Nobel Memorial Prize in Economic Sciences (1998) for his work on economic theories of famines and social justice and indexes for measuring the well-being of citizens in developing countries.

1942
Martin Cruz Smith, novelist (Gorky Park).

1949
Larry Holmes, professional boxer known as The Easton Assassin; his 20 successful defenses of his heavyweight title is second only to Joe Louis' record 25.

1952
Roseanne Barr, comedian, actress, producer; best known for her starring role in the TV series Roseanne, for which she won both an Emmy and a Golden Globe.

1952
David Ho, virologist, AIDS researcher.

1956
Gary Ross, film director, screenwriter (The Hunger Games, Seabiscuit).

NENO LA LEO; Kuhusu Dunia Kutokukuzuia.

The whole world steps aside for the man who knows where he is going.

Dunia nzima hukaa pembeni na kumpisha mtu anayejua anakoelekea.

Kuwa na ujasiri wa kujua unakoelekea na hakuna kitakachoweza kukuzuia.

Nakutakia siku njema.

Sunday, November 2, 2014

NENO LA LEO; Sehemu Ambapo Hofu Itakuwahisha.

Perpetual worry will get you to one place ahead of time - the cemetery.

Hofu ya kila mara itakusaidia kuwahi sehemu moja – kaburini.

Ni kweli hofu inaweza kukusababishia kifo.

Kuwa makini.

Nakutakia siku njema.

Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa Ni Muhimu Sana. Tuzingatie Mambo Haya Matano.

Tarehe 14/12/2014 itakuwa siku muhimu sana katika miaka mitano ijayo. Siku hii itakuwa ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa. Watu wengi sana hawaupi uchaguzi huu nafasi kubwa na wameelekeza macho na masikio yao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Hili ni kosa kubwa sana ambalo tunafanya watanzania wenzangu. Uchaguzi wa serikali za mitaa ni muhimu kama ilivyo uchaguzi mkuu. Ni kupitia serikali za mitaa ambapo tunakuwa na demokrasia ya moja kwamoja. Yaani kama kuna jambo lolote la kufanya maamuzi kwenye mtaa au kijiji basi wananchi wote watafanya maamuzi kwenye vikao na mikutano mbalimbali.

Pia serikali hizi za mitaa zina mamlaka ya kutunga sheria ndogo ndogo ambazo zinaweza kuwa na athari chanya au hasi kwetu sisi wananchi.

Serikali za vijiji zina mamlaka makubwa sana kwenye ardhi na hivyo zinaweza kufanya maamuzi ya kuuza ardhi kwa watu mbalimbali. Hivyo unapokuwa na serikali ya kijiji ambayo sio imara mnaweza kujikuta mnapoteza ardhi yenu.

Mwisho kabisa naamini mabadiliko na maendeleo ya nchi hii yanaweza kuanzia kwenye ngazi ya mitaa, vitongoji au vijiji. Hii ni kwa sababu matatizo yoyote tunayokumbana nayo kama taifa yanaanzia katika ngazi ya familia na hatimaye mitaa. Kwa mfano wahalifu wote wanaishi kwenye mitaa yetu, wauzaji wa madawa ya kulevya na hata watumiaji wanakaa kwenye mitaa yetu. Hivyo tukiweza kuwa na serikali zamitaa ambazo zipo imara tunaweza kujenga misingi mizuri kama taifa.

Baada ya kuona umuhimu huo mkubwa wa serikali za mitaa sasa naomba nikushirikishe mambo matano muhimu ya kuzingatia kwenye uchaguzi huu wa serikali za mitaa.

1. Hakikisha unapiga kura na hamasisha wengine nao wapige kura.

Ule utamaduni wetu watanzania wa kutokupiga kura halafu tunakuwa wa kwanza kulalamika kwamba viongozi ni wabovu sio utaratibu mzuri. Hakikisha unapiga kura siku hiyo ya uchaguzi na pia washawishi ndugu jamaa na marafiki zako nao wapige kura siku hiyo. Kura yako moja ina thamani kubwa sana, usiidharau.

uchaguzi

2. Chagua kiongozi mwenye maono na mwenye historia nzuri.

Kwanza kabisa mtu ambaye mtamchagua awe mtu ambaye mnamjua vizuri. Awe ni mtu ambaye amekaa kwenye mtaa huo na mna historia yake nzuri ya namna ambavyo amekuwa akihamasisha mambo mbalimbali kwenye mtaa au kijiji chenu. Awe ni mtu mwenye maono na anayefikiria na kukubali mabadiliko. Kiongozi wa aina hii ataweza kushirikiana nanyi kuleta maendeleo kwenye eneo lenu.

Kujua zaidi kuhusu tabia za viongozi bonyeza maandishi haya.

3. Mtu yeyote atakayotoa rushwa usifikirie mara mbili, usimpigie kura na hamasisha wengine wasimpigie kura.

Uongozi wa serikali za mitaa ni uongozi ambao hauna manufaa makubwa kifedha zaidi ya posho ndogo ndogo. Sasa mtu ambaye anatoa rushwa lili kupata nafasi hiyo, jiulize ananufaikaje? Kwa vyovyote vile atahakikisha akipata nafasi analipa fedha yake aliyowekeza kwa kutoa rushwa hivyo atawaingiza kwenye matatizo.

4. Chagua mtu, usichague chama.

Kwa siasa zetu za Tanzania bado haturuhusu mgombea binafsi hivyo unalazimika kuchagua mgombea anayeletwa na chama fulani. Chama kinaweza kuwa na sera nzuri sana ila kama kitakuwa na mgombea ambaye hana uwezo mzuri wa uongozi sera hizo ni kazi bure. Hivyo hudhuria mikutano ya kampeni, wafatilie vizuri wagombea wote na mchague mtu ambaye unaona anaweza kuleta mabadiliko kwenye mtaa au kijiji chenu. Hata kama wewe ni mkereketwa wa chama fulani ila ukaona mgombea wa chama kingine ana sifa zaidi ya mgombea wa chama chako, mpigie kura. Mwisho wa siku maendeleo yatakuwa ni kwa mtaa wenu na sio chama chenu.

5. Tuoneshe ushirikiano na kuwawajibisha viongozi tuliowachagua.

Baada ya uchaguzi na viongozi kupatikana ni vyema kuweka tofauti za kisiasa pembeni na kupeana ushirikiano ili kiongozi mliyemchagua aweze kutekeleza majukumu yake. Kwa kuonesha ushirikiano mzuri italeta mafanikio makubwa kwa mtaa au kijiji chenu.

Pia pale ambapo kiongozi mliyemchagua anakwenda kinyume na ahadi zake ni vizuri kumwajibisha. Kwenye serikali za mitaa tupo karibu sana na viongozi wetu na hivyo ni rahisi kuhoji mambo mbalimbali ambayo mnaona hayaendi sawa.

Nichukue nafasi hii kuwatakia watanzania wote uchaguzi mwema na twende tukafanye maamuzi sahihi kwa mitaa na vijiji vyetu kwa miaka mitano ijayo.

Tanzania ni yetu sote, tushirikiane kuijenga.